Yanga bado uswahili na ubabaishaji unatusumbua

Yanga bado uswahili na ubabaishaji unatusumbua

Sikutarajia kama Yanga ina watu wanafikiri vizuri hivi.
Mimi huwa nawaona yanga wote watupolo tu.Ila hapo umewaambia mkuu,kazi ni kwao kunyoa ama kusuka
Kiukweli ukiangalia namna GSM na viongozi wa Yanga wanavyoendesha timu kiukweli inashangaza sana. Nilitoa uzi hapa nikiziomba timu zetu zinazowakilisha nchi zijikite kwenye maandalizi ya uhakika kwa kucheza walau mechi zisizopungua nne ili kuimarisha vikosi na pia kuwaweka wachezaji katika fitness, lakini naona ni Simba pekee ndiye mpaka sasa ndio walionesha kuwekeza kwenye performance ya timu na huku Yanga ikionesha nguvu kubwa kuwekeza kwenye kupiga domo. Una mechi ya klabu bingwa mapema kabisa mwezi wa tisa lakini Cha ajabu hata haujacheza mechi yoyote ya kirafiki unaenda kuweka kambi Morocco kambi ambayo haina impact yoyote zaidi ya kupoteza muda.

Mechi ya wiki ya mwananchi haitokuwa na msaada wowote kiufundi kwasababu wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza watakuwa kwenye mataifa yao kucheza mechi za kimataifa. Na la pili hata yakionekana mapungufu una muda mchache sana kurekebisha kabla ya kucheza na Rivers United. Na hauwezi kujua kama imerekebishika pasipo kucheza tena mechi ya kirafiki kuona hali ya kikosi. Kwa upande wa maandalizi ya timu, GSM na viongozi wa Yanga wamefeli. Mimi binafsi ikitokea Yanga imeshindwa kuingia hatua ya makundi klabu bingwa sitolaumu mchezaji yeyote wala benchi la ufundi bali uendeshaji mbovu wa timu hakuna usiriazi kwenye uwekezaji wa uwanjani zaidi ya propaganda tu.

Kituko kingine ni hili la kumkaribisha Haji Manara ndani ya Yanga. Hili binafsi ni moja ya tukio lililonipa mashaka juu ya uwezo wa kufikiria kwa hawa watu wanaoionhoza Yanga. Yaani Manara katoa kila aina ya kejeli, kila aina ya tusi na hao hao Wana Yanga walikuwa wanapiga kelele kuwacheka Simba kuwa wanamsemaji mswahili sana lakini leo kageuka keki Yanga. GSM kawaza kibiashara zaidi lakini atambue kuwa hata Manara alivyokuwa yupo Simba, alifanikiwa kuujaza watu kwasababu ya mpira unaoonekana na matokeo yanayoonekana uwanjani na sio kwamba kupiga domo huku timu ikiwa haifanyi vyema.

Hivyo GSM na uongozi wa Yanga mpira sio kupiga domo na propaganda bali wekeni nguvu kwenye maandalizi ya timu, wekeni nguvu kwenye mpira mzuri na matokeo mazuri hata muhamasishaji hatotumia nguvu nyingi kujaza watu. Ila kama matokeo yatakuwa mabaya uwanjani huyo Manara hatoweza kuwafunga kamba watu wakajaze uwanja.

Mimi binafsi safari hii kama timu haitofika hatua ya makundi klabu bingwa, basi sina budi nikae pembeni ushabiki kwenye timu hii itakuwa basi tena nitarejea baada ya mfumo mpya wa uwekezaji.
 
Mkuu mtoa Mada unastahili uwe na blue tick you great thinker Hongera umewaza mbali
 
Huwa nasoma press za wenzetu huko kuhusu mechi zinazokuja, wenzetu ndio maana wameteka ulimwengu wa soka.

Kocha ndiye anayehusika kuzungumzia mechi maandalizi ya mechi hiyo, ila kwetu huku msemaji ndio anazungumzia ambapo hajui hata kocha kaandaaje wachezaji
Utamaduni hauwezi lingana.
Hata kwenye imani tamaduni za eneo husika zipo.
 
Nimemsikiliza leo msemaji mpya wa hawa unaowazungumzia nikaona kuna shida yaani press karibu yote ni kuzungumzia ubaya wa alipotoka badala ya kuzungumzia mipango na nini atafanya alipo ni vijembe tu na blahblah

Lilipoulizwa swali kuhusu hiyo mechi na hao wanaijeria ndiyo nikaona hawa watu wategemee maumivu wakijitahidi sana hapa watatoa draw
Haji yuko bize kutoa mipasho kwa Simba, wakati Simba wao wala hawahangaiki kumjibu. Wanachofanya ni kutoa taarifa ya uzinduzi wa App mpya na taarifa ya mechi nyingine ya Pre- season.

Ndio mtajua wenzenu wapo next level. Huko mlipo wenzenu wameshatoka.
 
Muda sio mrefu tutaimba parapanda kwa uto
Wanazidiwa akili hata na timu ya Biashara na Azam fc ambao wako bize kuandaa vikosi vyao kwa kutafuta muunganiko na fitness kwa kucheza mechi za majaribio. Timu ya Yanga imekuwa kubwa jinga
 
Nilizungumza hapa sasa madhara ya kutocheza mechi nyingi za majaribio leo majibu yamepatikana. Na siku za kucheza klabu bingwa zinahesabika. haujacheza mechi hata moja ya majaribio unakuja kucheza mechi na Zanaco ambao wameshacheza mechi tisa za majaribio
 
Tulieni hivyo hivyo dawa iendelee kuwaingia vizuri.

Mnajitekenya wenyewe na Kujichekesha wenyewe

Kama ninyi mnaendelea na kambi, kitu gani kinachokufanya ufatilie mambo ya Yanga,kila mmoja ashinde mechi zake na afanye mambo yake anayo ona ni ya msingi

Mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu
dawa leo imetuingia vizuri mkuu
 
Nilizungumza hapa sass madhara ya kutocheza mechi nyingi za majaribio leo majibu yamepatikana. Na siku za kucheza klabu zinahesabika. haujacheza mechi hata moja ya majaribio unakuja kucheza mechi na Zanaco ambao wameshacheza mechi tisa za majaribio
Ile ya dtb kigamboni haikuwa mechi
 
Nilizungumza hapa sass madhara ya kutocheza mechi nyingi za majaribio leo majibu yamepatikana. Na siku za kucheza klabu zinahesabika. haujacheza mechi hata moja ya majaribio unakuja kucheza mechi na Zanaco ambao wameshacheza mechi tisa za majaribio
Amken amkeni. Mitambo imelipuka huku Wamepigwa tenaaaaa. Mdomo umewaponzaaa
 
Back
Top Bottom