John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Wanafainali wa michuano ya Kombe la FA msimu uliopita, Yanga, leo saa moja usiku watakuwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kutafuta nafasi ya kutinga Hatua ya Robo Fainali wakati itakapocheza dhidi ya Biashara United kutoka mkoani Mara.
Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alinukuliwa hivi karibuni akisema kuwa timu yake inafanya maandalizi ya mchezo huo Pamoja na mwingine wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Februari 23 kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Biashara imekuwa na mwenendo wa kusuasua katika Ligi Kuu msimu huu.