Yanga dirisha dogo la usajili Fanya haya

Yanga dirisha dogo la usajili Fanya haya

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Dirisha dogo la usajili linakuja January
Yanga Bado tuna kikosi kizuri mno
Naomba viongozi msivunje timu Kwa kuingiza wachezaji wengi

1. Mtoe kasi ya Baleke au Msonda ili muingize kiungo mkabaji aje kumsaidie Aucho ambayo energy yake inashuka

2 Beki wa kulia wa ndani ya nchi
Yao hana mbadala naona Gamond hamuamini Kibwana japo ya kuwa beki mzuri, labda mifumo ya Gamond imegoma
Nenda pale Azam mlete Paschal Msindo au Chilambo

3 Kwa striker Bado Nina Imani kubwa na Dube, nadhani Kuna vitu anatakiwa aviboreshe ili awe Bora zaidi

4. Mkataba wa Chama unaisha mwisho wa msimu, mpenzi mkono wa kwaheri, ili muingize winger hatari

5. Kibabage nafurahia energy yake anakimbiza mno, aboreshe cross ya mwisho atakuwa beki mzuri

6. Punguza rundo la wachezaji, au watoe Kwa mkopo akina Kibwana, shekhan, Mshery Farid n.k watafue changamoto mpya hapo wataharibu vipaji vyao
 
Simba ndo wateja wakuu wa yanga. Vipi nanyi huwa mnalipwa sh ngapi ili muwe mnadai kusomewa kwenye mikutano kwamba yanga ni chanzo Cha mapato yenu.
Una uhakika umetandika kitanda shuka au umekurupuka umesikia mdundiko!
 
Back
Top Bottom