Yanga haitapata kitu kuuzwa kwa Msuva Benfica

Yanga haitapata kitu kuuzwa kwa Msuva Benfica

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Yanga wakati wa kumuuza Msuva 2017 Difaa El Jadida walishauriwa na meneja wa Msuva wamuuze dola 80,000 (Tsh mil 180) ili waweke kipengele cha kupata mgao akiuzwa kwingine (Benfica) ila walikataa na kulipwa dola 100,000 (Tsh mil 229) hivyo hawana mgao wowote
IMG_20200107_211716.jpeg
 
Dah hizi roho zetu acha ziendelee kulaaniwa, yani badala ya kupongeza umekuja kuanzisha thread kwa mtindo wa malalamishi.
Onesha lawama hapo, nimeleta Uzi maana kuna maswali yanaulizwa kuhusu hili

Mimi kama mwanaspoti nimejitokeza kutolea ufafanuz ,unasema nalaumu?

Binafs mm ni Yanga fan
 
Kwani mpira wenyewe wanauchezea mda gani?
 
Sisi watu wa mahesabu tutaangalia hiyo tofauti ya M31 na pesa yoyote ambayo yanga wangeipata kuanzia kwa benfica na kuendelea ,tukizingatia Present Value na time value of money kisha tutarudi kutoa hitimisho kati ya nanager wa mchezaji na team nani ni mbumbumbu
 
Milioni 229 unanunua wachezaji kibao local..nani alijua ataenda Ureno
Hawa ma mbumbumbu ni shida sana.

Wanajaribu kumlinganisha na Mbwana Samatta ambaye aliwagomea kucheza kwa kushindwa kumpa gari Mark II waliyokuwa wameahidi.

Nani kasema mkataba lazima uwe na kipengele hicho?
 
Sio tamaa ni ubinafsi wa viongozi wa yanga walitanguliza maslah yao mwenyewe kwa sababu walijua hawatakua viongozi tena hivyo kiongozi atakae kuja hawata nufaika na chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye mkataba wa kuuzia Kati ya Yanga na Wamorocco kuna kipengele kinasema Yanga itapata 20% ya hela pindi Msuva atakapouzwa timu nyingine.

Sent from my TA-1024 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom