Yanga hakuna timu

BETONY

Senior Member
Joined
Apr 4, 2012
Posts
188
Reaction score
170
Yanga imekuwa na mwendo wa kusuasua toka msimu mpya umeanza. Ilijitapa kw usjili wa mafungu mafungu. Mpaka sasa hakuna mchezaji aliyesajiliwa na kuonesha kiwango kikubwa.
Timu haina chemistry, haiwezi piga pasi mbili kwa usahihi.
Kocha Zahera ameshindwa kutengeneza muunganiko wa timu.
Namtabiria Mwinyi Zahera kufukuzwa mapema sana.
Mechi zaidi ya tano hajaweza tatua tatizo la umaliziaji kwa washambuluaji wake
 
Tengeneza ya kwako
 
Kwaiyo unataka zahera aingie akafunge? Timu ilikua haina uwezo wa kutengeneza nafasi, kwasasa timu inapata nafasi ila kumalizia ndio tatizo sasa Zahera utamlaaumu vip? Wachezaji husika wanatakiwa waonyeshe kama wanastahili kucheza Pale mbele.
 
Mtoa mada ni mtu ambaye hujui mpira, timu yetu ipo vizuri sana hasa upande wa kati na mabeki, shida ni mbele ila tatizo litaisha tu, Kumbuka timu ni mpya kwa hiyo muunganiko ndio unaendelea kutengenezwa, ingawa nina wasiwasi na Kalengo na Bigirimana
 
Shida foward hivi kweli yanga muda wote huo wameshindwa pata kibali cha molinga
 
Shida foward hivi kweli yanga muda wote huo wameshindwa pata kibali cha molinga
Idadi ya wachezaji itaongezwa kama itafuzu makundi ya champions league au ya shirikisho.Huenda Moringa ataongezwa au atasajiliwa mwingine mpya tu
 
Yanga haina Chemistry ila huko Umbumbumbuni kuna Biology, Mathematics hadi History ndio maana mliwatoa Wamakonde.

Tatizo Bongo kila mtu ni kocha na anaujua mpira.
 
Yanga haina Chemistry ila huko Umbumbumbuni kuna Biology, Mathematics hadi History ndio maana mliwatoa Wamakonde.

Tatizo Bongo kila mtu ni kocha na anaujua mpira.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu umenifanya nicheke kwa nguvu,maana tokea mechi iishe ndo nacheka nao
 
vyura hao kila ukiwambia timu haiko vizuri wanakwambia timu ni mpya bado muunganiko, mara zahera hakuwepo kwenye kipindi cha Pre season, pumbaaaaaaaa!!!!
 
vyura hao kila ukiwambia timu haiko vizuri wanakwambia timu ni mpya bado muunganiko, mara zahera hakuwepo kwenye kipindi cha Pre season, pumbaaaaaaaa!!!!
Mikia Hanna mamlaka ya kuongelea Yanga CAF champions league...mmetoka awali kabisa Kama timu za Somalia..Yanga haijawahi kutolewa mechi za awali
 
Kwa anayejua mpira na akachambua mpira basi ataongea kimpira, jana yanga imecheza vizuri sema tatizo fowadi umakini bado ila imebadilika sana Yanga hasa beki na middle
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…