Yanga hakuna timu

Nauza yanga mbovu na chuma chakavu
 

simba au azam yenye kocha bora imefika wapi
 
simba imefika wapi yenye mwendo usikuwa wa kususua
 
Kwa anayejua mpira na akachambua mpira basi ataongea kimpira, jana yanga imecheza vizuri sema tatizo fowadi umakini bado ila imebadilika sana Yanga hasa beki na middle
38% possession ndio vizuri?
 
sio kwamba hakuna timu bali bado kocha ana kazi ya kuwaweka sawa na nina amini atafanikiwa
 
Tangu msimu wa Ligi uanze Yanga imecheza mechi nne. Niambie kati ya hizo ipi imedhihirisha kwamba Yanga ni timu ya kubezwa na hiyo unayojivunia ni timu ya kuogopwa?
Yanga 1 - Township Rollers 1 (Dar). Unakusudia mechi hii? Kama ni hii basi hata hiyo unayoidhania ni timu yako nzuri basi ni mbovu, maana nayo ilicheza na Rollers hii hii Afrika ya Kusini na matokeo yakawaje? 1-1 hiyohiyo!
Township Rollers 0 - Yanga 1 (Gaberone). Unakusudia mechi hii? Unakusudia Township Rollers iliyotoka 1-1 na timu unayoiona ni kabambe ni mbovu mno hadi ikafungwa goli moja na Yanga? Kama Yanga kuifunga timu hii ni udhaifu, basi hiyo timu yako iliyotoka nayo sare ni dhaifu zaidi. Au ulikusudia ili Yanga iwe nzuri basi ilihitaji lazima kutoka sare ya 0-0 kama hiyo timu unayoiona nzima ilivyofanya ugenini Msumbiji?
Ruvu Shooting 1-Yanga 0. Unakusudia mechi hii? Tangu lini timu kufungwa 1-0 na timu nyengine ya Ligi hiyohiyo ikawa ndio kigezo cha ubovu? Hiyo timu unayiona ni kabambe inapofungwa na Kagera na Toto kila kwenye Ligi nayo ni mbovu pia?
Yanga 1-Zesco1. Unakusudia mechi hii? Kigezo cha ubovu ni udhaifu wa Zesco? Mbona mlisema Yanga ingebugia hata bao 5 kabla ya mechi? Au udhaifu ni sare ya 1-1? Mbona hayo hayo ndiyo matokeo ya mechi baina ya hiyo timu yako kabambe na UD Songo, na bado Yanga hawajasema kuwa timu yako ni mbovu?
Bado sijakuelewa.
 
Tatizo ukiambiwa Yanga ni timu mbovu, unalinganisha na mechi za Simba! Tena unalinganisha na mechi za Simba baadhi yake ni za zamani enzi zile Toto Africa haijashuka daraja! Angalia uchezaji wa timu, uangalie spirit ya uchezaji, upime kama kuna room kwa timu kuja kuwa nzuri hapo baadaye au la! Ukilinganisha mechi za Simba na Yanga utaiona Yanga iko chini sana, unachotakiwa ni kuangalia muendelezo wa improvement za uchezaji, sio mechi huku ya Yanga, kule ya Simba!
 
Atafukuzwaje wakati ndo sponsor ?? Especially kwenye wkt mgumu anatoa hela yake anawapa wachezaji wanakula,kwenye kubwa kuliko anachanga $500/= mtu km huyo hawezi fukuzwa maana kazi yake kufundisha wachezaji ndo wao kazi yao kupeleka uwanjani wanachofundishwa na mwl wao ...haya mawazo tukiwa tunapindua meza lakini mkeka usipopinduka ndukiiiii
 
Kwani kuna katazo ni vigezo gani vilinganishwe na vipi visilinganishwe? Hewalla, tuondoe hizo ‘baadhi’ unazosema ni za zamani, tubaki na ’baadhi’ ya hizo za sasa hivi. Pia tusilinganishe? Kwani mechi unazozitumia kuinanga Yanga nazo si ‘baadhi’? Au ‘baadhi’ inayokatazwa ni ya mechi za Simba tu?
Umezidi kuwa hueleweki!
 
We mwenye timu bora umekuwa kikundi cha ushangiliaji huoni tofauti?
 
Kwa ujumla bongo hakuna mpira ila watanzania wanajifariji tu na kile walichonacho, ndio maana ukigusia vibaya kinachowafariji lazima wawe wakali.
 
Shida foward hivi kweli yanga muda wote huo wameshindwa pata kibali cha molinga

Ninayofahamu mimi jukumu la kuomba kibali siyo la Yanga bali ni la TFF...Yanga kazi yao ni kupeleka jina TFF abao ndio wanaowasiliana na CAF...I stand to be correccted
 
... Kwani mechi unazozitumia kuinanga Yanga nazo si ‘baadhi’? Au ‘baadhi’ inayokatazwa ni ya mechi za Simba tu?
Umezidi kuwa hueleweki!
Leta mechi za msimu huu tangu unaanza, kuanzia za kirafiki, ligi ya bara hadi CAF. Simba haijapoteza hata mechi moja msimu huu. Yanga amepigwa na Polisi na Ruvu Shooting.
 
Leta mechi za msimu huu tangu unaanza, kuanzia za kirafiki, ligi ya bara hadi CAF. Simba haijapoteza hata mechi moja msimu huu. Yanga amepigwa na Polisi na Ruvu Shooting.
Unakijua unachoongea Lakini? Mechi ya Yanga na Polisi ni ya Ligi? Ni ya msimu huu? Kama ni hivyo, Mbona umekataa kuhusishwa mechi ya kirafiki ya Simba na Township Rollers? Mbona hizo za CAF hutaki kujua kwamba hiyo nzima yako yenyewe imeshatolewa ilhali hiyo mbovu inaendelea? Zitapatikanaje mechi za Msimu huu wakati Yanga haina mechi za Msimu huu wa Ligi, ina mechi ya Msimu huu tu? Umejitahidi, lakini bado hujaeleweka.
 
Nimekuambia msimu huu kuanzia za kirafiki, ligi ya bara na za CAF. Rudi tena ukasome vizuri. Au unataka kusema mechi ya Polisi haikuwa katika mechi za kirafiki kujiandaa katika msimu huu?
 
Yanga haijawahi kutoka hatua ya awali CAF champions league..hiyo level ya timu za Somalia..sasa ubora wa mikia huko wapi
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…