Yanga hali si shwari hata kidogo

Yanga hali si shwari hata kidogo

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Kutokana na kipigo mfululizo kila yanga inapokutana na Simba na hasa hiki cha juzi Yanga ikiwa kwenye ubora wake kutokana na kuwa na wachezaji wengi wenye kulipwa mapesa mengi na pia kuwa katika nafasi nzuri sana katika ligi. Hali kwa team Yanga imekuwa yenye mashaka huku vikao vikiendelea chinichini akitafutwa nani mchawi au wa kutolewa kafara kutokana na hali hii. Usiku wa jana matawi ya yanga ya Magomeni, Sinza, Kimara, Ilala na Kinondoni kwa kutumia wawakilishi walikutana moja ya hotel zilizopo Sinza barabara ya Sam Nujoma kwa ajili ya miakati mbalimbali.

Watu hawa ambao inasemekana wanafadhiliwa na bwana mmoja mwenye pesa ambaye nadhani sasa ni wakati wake kuchukua team kwa kuwa amekuwa akisisitiza kuwa yanga haishindi kwa sababu ya kuwa na uongozi mzuri isipokuwa rushwa kutumika kwa baadhi ya mechi. Bwana huyo amekuwa akitoa ushahidi ambao wengine tunashindwa kuuamini kama ni kweli au si kweli akitaja mechi na wachezaji ambapo "inasemekana "walihusika kuzihujumu team zo zifungwe na yanga ili kuhalalisha uongozi uliopo madarakani. anasema imekuwa ngumu kufanya hivyo wanapokutana na simba kwa sababu ambazo nmeona nisizitaje.

Moja ya mambo yanayopigiwa kelele sana ni kitendo cha yanga kusajili wachezaji wengi toka simba kuwa ni moja ya mambo ambayo yatakuja kuwasumbua hapo mbeleni. Akitoa mfano wa kuwa hata okwi ambaye alisajiliwa kwa mbwembwe na tambo nyingi sana alikuwa tofaut alipokuwa akichezea yanga na sasa anapochezea simba.

Mzee mmoja maarufu ambaye pia inasemekana amekuwa na mkono wa chinichini katika jambo hili alisikika akilalamika kuwa wao wamekuwa na Simba B tena Veteran. Kwa maana ya kuwa team ya simba imekuwa mara zote ina waingiza mkenge kwa mpango ambao yeye ameuita wa siri. Simba hujidai inataka kumwongezea mkataba mchezaji wao fulani kwa dau ambalo huwa wanakuwa kama wanasita sita ili yanga wajitokeze wawapiku na hivyo yanga ionekane imewakomoa simba na matokeo yake huwa siku zote wachezaji hao wanaenda yanga wanachuma na baadaye kurudi simba au kundelea na maisha mengine.

Yanga ambayo sasa inajiandaa na mech ya kimataifa dhidi ya platinum toka zimbabwe inajitahidi sana kuficha jambo hili ili kutovuruga saikolojia ya wanachama na wachezaji. ila kiukweli kuna wachezaji ambao wametajwa kuonekana kama ni kikwazo kila mara kwa yanga kupata ushindi.

Mimi ningependa kuwashauri yanga watulie waangalie mechi zilizopo mbele yao kufungwa si jambo geni na kwa sasa hata sisi mashabiki tumezoea kuwa tukijitahidi sana na simba ni kutoa draw.

Mpira una mambo mengi tujitahidi kufanya usajili wa nguvu na utulivu hapo mbeleni tuache kudandia wachezaji wa simba
 
tumechoka...nikweli kabisa tumechoka!sisi inamaana hatuoni wachezaji wengine hadi haya makapi ya simba!si bure tumelogwa kwa kweli...au la tunajikaanga wenyewe
 
Hamna ujanja kwa kutafuta wachezaji. Mnangoja Simba wawachoke ndio msajili makapi.
 
tumechoka...nikweli kabisa tumechoka!sisi inamaana hatuoni wachezaji wengine hadi haya makapi ya simba!si bure tumelogwa kwa kweli...au la tunajikaanga wenyewe
Usisahau kama hayo makapi ya Simba ndo yameifanya timu ya Yanga iongoze ligi hadi leo na makapi hayo hayo ndo yameifanya Yanga ifuzu hatua inayofuata ya mashindano ya kombe la shirikisho la Afrika.
 
jana nimecheka sana kumsikia david mwakalebela alishauri wachezaji wa yanga wafukuzwe nikasema mbona yeye alipokosa penati zanzibar tena alikuwa akiogopa kupiga wakati wa mechi ya fainali ya kombe la afrika mashariki hakuna mtu aliyemnyooshea kidole kuwa kahongwa kweli yanga wamechanganyikiwa
 
Masuke kuna siri kubwa sana kwenye ushindi wa Yanga. hilo washabiki wengi hawajui. kuna match tunashinda kuna match tunanunua. mi nakwambia hilo kwa kuwa yanga haichezi kama team yanga inacheza kutegemea mchezaji mmoja mmoja na kuna kipindi kabisa kunakuwa na mipango nani aachiwe kufunga magoli na team pinzani ili ionekane tumefanya usajili mkubwa sana. kinachoendelea yanga ni siasa kama ambavyo simba inafungwa au kutoa draw si kwa sababi ni team mbovu ila kuna siasa ndani yake. na watu wenye akili ndo hofu yao ipo hicyo kuwa skama simba itatulia baada ya mwaka itakuwa team nzuri sana . na kumbuka simba haisajili kwa gharama sana. wakati yanga tunahangaika na gharama kubwa na bado tunafanya fitna kushinda....
 
wewe ni muwongo vikao vinafanyika ni kupanga mikakati ya mechi na wazimbabwe leo tulikaa
 
wakimataifa ungekaa kimya wala tusingejua kuwa hujui.

mimi nakwambia kitu ninacho kifahamu maana kama kikao cha mikakati nakifahamu na ninavyokwambia navifahamu sasa wewe sema mimi muongo mpaka yatokee ya kutokea.

na ujue hii mechi ya wazimbabwe imewekwa kimtego mtego sana kuwa kama tukipoteza hapo ipatikane sababu kubwa zaidi na kitu ambacho manji hatak kitokee kwa kuwa yanga anataka aitumie imsaidie kwenye harakati za kugombe ubunge mwaka huu. so inabdi pia ichukue kombe...

wewe ambaye hujui ila inadhani unajua ni mbaya kuliko yule ambaye hajui na anajua kuwa hajui. wewe subiri mimi nmeonya hili kwa manufaa ya club ili isishindwe. nasi tumechoka mtaan tunazodolewa tu na wanasimba kwa kutuita majina ya ajabu ajabu... lazima kuna kitu.
 
Masuke kuna siri kubwa sana kwenye ushindi wa Yanga. hilo washabiki wengi hawajui. kuna match tunashinda kuna match tunanunua. mi nakwambia hilo kwa kuwa yanga haichezi kama team yanga inacheza kutegemea mchezaji mmoja mmoja na kuna kipindi kabisa kunakuwa na mipango nani aachiwe kufunga magoli na team pinzani ili ionekane tumefanya usajili mkubwa sana. kinachoendelea yanga ni siasa kama ambavyo simba inafungwa au kutoa draw si kwa sababi ni team mbovu ila kuna siasa ndani yake. na watu wenye akili ndo hofu yao ipo hicyo kuwa skama simba itatulia baada ya mwaka itakuwa team nzuri sana . na kumbuka simba haisajili kwa gharama sana. wakati yanga tunahangaika na gharama kubwa na bado tunafanya fitna kushinda....

Kwa hiyo unamaanisha Yanga haina uwezo wa kushinda mechi kwenye hii ligi ya Vodacom?
Coast,Prison,Mtibwa hawa wote walipewa hela?
 
Kuna wadau muhimu humu kama Makoye Matale siwaoni kabisa tangu Jumamosi kabla ya mechi. Ni vizuri tukabadilishana mawazo ili walau tupate sare kwenye mechi za Simba
 
kuna mechi inashinda kuna mech Yanga inahonga na ktk hizo ulizotaja mechi ya Coast na Mbeya city tulinunua wachezaji.

kutokana na ugumu wa mechi zenyewe na nafasi tulikuwa tunahitaji sana. na mwaka huu ni lazima yanga wachukue kombe kumjenga kisiasa manji.

athari zake ni kuwa ni sawa na mwanafunzi ambaye unamwibia mitihani ili afaulu. unategemea nini baadaye atakapoonekana anastahili kwenda chuoni na akapata degrees zake? tungekaa kuijenga yanga ya leo na kesho kama team kama team ya kudumu. tunapokimbilia kununua wachezaji wa simba kila mara akiondoka manji tutakuwa na team gani? maana usisahau yeye ndo anayenunua wachezaji hawa.

mi nakwambia kama simba wasingekuwa na migogoro wana team na kocha mzuri sana, sema tu watani wetu hawajasetle ndani kwao na tuombee hivyo
 
we nyenyere wabotswana uliona team pale?

hivi unadhan tungekutana na el mereikh ingekuwaje? hata hawa platinum tunawaondoa hamna team pale.

team ambayo ilishika nafasi ya nne zimbabwe na haijawah kushiriki mashindano yoyote isipokuwa haya ndo mara ya kwanza? kuna mechi tunashinda sikatai,kuna mechi tunanunua hasa za ndani na za east afrika kama mwaka ule tumechukua kombe ili tupate nafasi ya kwenda kuonana na kagame.unajua tulitumia nguvu kubwa ya pesa kushinda lile kombe ili liwe sababu ya kwenda kuonana na kagame? unajua lengo lilikuwa ni nini?

baada ya kagame kutokukubalia tulichotaka ndo tukaanza mizengwe kushiriki kombe la kagame. wewe mshabiki hujui kinachoendelea huku ndani.

na ndo maana wenye akili huwa hata hawazimii wanaozimia ni wale wenzangu na mimi ambao hawajui kitu....
 
Chizi Maarifa;

Mweeeeh!
Ila Manji haaminiki!
Kama hata waandishi wa habari anawanunua atashindwa kununua game??
 
Last edited by a moderator:
Hizi ni story za kinafiki.

Hivi hao wachezaji wamesajiliwa jumapili? Na kama walisajiliwa zamani kwanini hatukusema haya? Kwanini hatukusema haya wakati tunashinda? Tuangalie maslahi mapana ya timu: 1: Kombe la Shirikisho 2: Ubingwa ligi ya Tanzania. Ligi ikiisha tutajadilia haya kwakua kuna muda wa usajili. Sasa hivi kuanza haya maneno ni majungu na fitna zinazoweza athiri timu.Tuwe makini na maadui zetu waona weza kutumia huu mwanya kutugombanisha ili wao wawe juu yetu kwenye ligi. Ila kama kuna watu wanatafuta faida zao binafsi waendelee kuleta chokochoko na sisi kama hatufikirii tuwonge mkono ili miwsho timu ikose kila kitu ndio tufurahi.

Mechi imekwisha matokeo yameonekana tunatakiwa kusonga mbele na kuziba mapengo kwa uangalifu tukiangalia majukumu yaliyo mbele yetu sio kuharibu. DAIMA MBELE NYUMA MWIKO. Tusiikane kauli mbiu yetu
 
Back
Top Bottom