Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Kutokana na kipigo mfululizo kila yanga inapokutana na Simba na hasa hiki cha juzi Yanga ikiwa kwenye ubora wake kutokana na kuwa na wachezaji wengi wenye kulipwa mapesa mengi na pia kuwa katika nafasi nzuri sana katika ligi. Hali kwa team Yanga imekuwa yenye mashaka huku vikao vikiendelea chinichini akitafutwa nani mchawi au wa kutolewa kafara kutokana na hali hii. Usiku wa jana matawi ya yanga ya Magomeni, Sinza, Kimara, Ilala na Kinondoni kwa kutumia wawakilishi walikutana moja ya hotel zilizopo Sinza barabara ya Sam Nujoma kwa ajili ya miakati mbalimbali.
Watu hawa ambao inasemekana wanafadhiliwa na bwana mmoja mwenye pesa ambaye nadhani sasa ni wakati wake kuchukua team kwa kuwa amekuwa akisisitiza kuwa yanga haishindi kwa sababu ya kuwa na uongozi mzuri isipokuwa rushwa kutumika kwa baadhi ya mechi. Bwana huyo amekuwa akitoa ushahidi ambao wengine tunashindwa kuuamini kama ni kweli au si kweli akitaja mechi na wachezaji ambapo "inasemekana "walihusika kuzihujumu team zo zifungwe na yanga ili kuhalalisha uongozi uliopo madarakani. anasema imekuwa ngumu kufanya hivyo wanapokutana na simba kwa sababu ambazo nmeona nisizitaje.
Moja ya mambo yanayopigiwa kelele sana ni kitendo cha yanga kusajili wachezaji wengi toka simba kuwa ni moja ya mambo ambayo yatakuja kuwasumbua hapo mbeleni. Akitoa mfano wa kuwa hata okwi ambaye alisajiliwa kwa mbwembwe na tambo nyingi sana alikuwa tofaut alipokuwa akichezea yanga na sasa anapochezea simba.
Mzee mmoja maarufu ambaye pia inasemekana amekuwa na mkono wa chinichini katika jambo hili alisikika akilalamika kuwa wao wamekuwa na Simba B tena Veteran. Kwa maana ya kuwa team ya simba imekuwa mara zote ina waingiza mkenge kwa mpango ambao yeye ameuita wa siri. Simba hujidai inataka kumwongezea mkataba mchezaji wao fulani kwa dau ambalo huwa wanakuwa kama wanasita sita ili yanga wajitokeze wawapiku na hivyo yanga ionekane imewakomoa simba na matokeo yake huwa siku zote wachezaji hao wanaenda yanga wanachuma na baadaye kurudi simba au kundelea na maisha mengine.
Yanga ambayo sasa inajiandaa na mech ya kimataifa dhidi ya platinum toka zimbabwe inajitahidi sana kuficha jambo hili ili kutovuruga saikolojia ya wanachama na wachezaji. ila kiukweli kuna wachezaji ambao wametajwa kuonekana kama ni kikwazo kila mara kwa yanga kupata ushindi.
Mimi ningependa kuwashauri yanga watulie waangalie mechi zilizopo mbele yao kufungwa si jambo geni na kwa sasa hata sisi mashabiki tumezoea kuwa tukijitahidi sana na simba ni kutoa draw.
Mpira una mambo mengi tujitahidi kufanya usajili wa nguvu na utulivu hapo mbeleni tuache kudandia wachezaji wa simba