Yanga hamjakurupuka kumfukuza Zahera?

Yanga hamjakurupuka kumfukuza Zahera?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Siyo jambo la ajabu kocha kufukuzwa kwenye club timu ikikosa matokeo viwanjani, lakini hii ya Zahera kushindwa kuifunga Pyramids na Ruvu kustahili kufutwa kibarua hainiingii akilini.

Pyramids ina uwezo mkubwa uwanjani na nje ya uwanja kuliko timu yoyote kwenye ukanda wa CECAFA. Yanga ndiyo timu Tanzania ambayo wachezaji na benchi la ufundi wanaidai club hela zao. Yanga ndiyo timu ambayo ina wachezaji ambao pamoja na kuonekana kwenye club ya Yanga, lakini hawaruhusiwi kucheza mashindano ya kimataifa. Yanga ni timu ambayo ina wachezaji muhimu wagonjwa kwa muda mrefu. Yanga ilikuwa na wachezaji muhimu wenye kadi za njano na nyekundu kuelekea mechi ya marudiano na pyramids huko Misri.

Hivyo, hata umlete Zenadine Zidane Yanga lazima Yanga ingefungwa na Pyramids tu. Sawa na Man U na Arsenal kuwafukuza Mourihno na Wenger lakini vipigo vikaendelea kubaki palepale.

Nadhani viongozi wana shida nyingine na Zahera, siyo kufungwa na Pyramids na Ruvu Shooting.

Nadhani tabia ya Zahera ya kupenda kuongea na kuanika ukweli ndani ya club hatujaizoea.
 
mimi mwanayanga.. ila najua kufukuzwa kwa zahera tatizo bado hatujalitatua... sitashangaa simba wakitufunga 5-0.. na ligi tukafanya vibaya sana
 
Ngoja tusubiri muda utasema.

ila

Huyu Dr Mshindo msola tutamkataa wenyewe anang'hata nakupuliza.
 
Mkuu Muida utaamua, kuna watu wanaficha madhaifu yao. hawa viongozi wamekurupuka na watalipia hili wape muda.
 
Kama ni kufungwa kwenye ligi hata Simba na Azam pia zimefungwa, na kama ni kutoka na ushindi mwembamba, 1-0 hata Simba na Azam pia mwendo ni huohuo. Viongozi wasitufanye wajinga Sisi, ni nini hasa Zahera amekosea?

Kuwakosa akina Boxer, Mohamed Banka, Kelvin Yondan, Molinga, na wale wote wa kimataifa kwampigo kwenye mechi ni pigo Kwa timu na kocha, ni Sawa na Simba bila Kagere, Barca bila Messi, Liverpool bila Salah na Mane kwenye mechi.

Nadhani maelezo ya kina yanahitajika hapa sio kama hivi
 
Yaani hapo ulipoifananisha simba na yanga ndipo ulipojichanganya ? Unapata wapi ujasiri wa kufananisha matokeo ya simba na chura?
 
Si mmefungwa na Mwadui na UD Songo pia au..?
 
Mi naona sawa tu walivyotemana naye! Katika soka hili ni kawaida! Ni heri kuziba ufa kuliko kungojea kuta zibomoke! Hawa Mikia kabla ya Uchebe karibu kila msimu walikuwa wakibadili makocha! Eti na wao wanashangaa.......! Zahera sio kocha wa kwanza wala wa mwisho kufukuzwa Yanga!
 
Mlipeni pesa zake...madhulumati nyie.majizi na majambawazi makubwa.mtu amewafadhili leo hii mnamfanyia hivyo.kweli mfadhili mbuzi unaweza ukampika ukapata nyama na mchuzi binadamu utaambulia mashuzi tu. Mpeni pesa zake.na dante alipwe pesa zake pia.dada nlikuwa nakuheshimu sasa nmekuja gundua nawe mwizi ñmesikitika sana

Mi naona sawa tu walivyotemana naye! Katika soka hili ni kawaida! Ni heri kuziba ufa kuliko kungojea kuta zibomoke! Hawa Mikia kabla ya Uchebe karibu kila msimu walikuwa wakibadili makocha! Eti na wao wanashangaa.......! Zahera sio kocha wa kwanza wala wa mwisho kufukuzwa Yanga!
 
Timu ikipata matokeo mabaya chini ya Mkwasa bakora hazitaepukika
 
Kiufupi kuondoka kwa zahera sio solution ya kutatua tatizo wataendelea kupata matokeo mabaya
 
Ubaridi wa yanga ndiyo tatizo, mli waachia simba wakateka media zote, waka seti na ajenda dhidi ya zahera, media zote zikawa ni zahera kasema hiki zahera kasema kile mpaka wimbo ukaingia masikioni mwa watu hata wasiyojua mpira. Kumbuka kauli ya manara alipotabiri kufukuzwa kwa zahera, tff kutunga kanuni mahususi ya kaptura.
Kuna msemo maarufu wa ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya, na hivyo ndiyo iliyo tokea. Fuatilieni thread za akina genta, Eagle, gwazat, okwiboban na wengineo za siku zilizo pita na za sasa.

\

Simba wanayo kete moja tu ya kusogeza mbele, nayo ni Mo tu baasi. Kete ya Yanga ilikuwa Manji, ilivyoliwa basi na bao likaishia hapo. Sasa hivi karibu wachezaji wote wanaidai club ya Yanga hadi wengine wamegoma wakidai 40m zao.

Mkwasa alishakuwepo Yanga kama kocha na kama kiongozi bila kuonyesha chochote cha maana kwenye club eti sasa wamemrurisha kuwa mkufunzi, huku ni kurudi nyuma, ni afadhali hata ya Masoud Djuma kuliko Mkwasa.
 
Kiufupi kuondoka kwa zahera sio solution ya kutatua tatizo wataendelea kupata matokeo mabaya
Ni lazima wanachama na shabiki tujulishwe ni nani alisababisha wachezaji kukosa vibali vya kucheza mechi za kimataifa? Ni lazima tujuzwe pia ni wachezaji gani wanadai hela ngapi? Ilikuwaje Ajibu, Makambo, Gadiel na Haji Mwinyi wakaachwa waondoke huku klabu ikiwa inawahitaji?
 
Shida yetu watu wengi ni mashabiki oya oya... Nahili si kwa yanga peke yake.

Back
Top Bottom