Yanga hatarini kufungiwa usajili, Eymael asema asilaumiwe

Yanga hatarini kufungiwa usajili, Eymael asema asilaumiwe

Sasa wataporwaje pointi 9 kwenye ligi ambayo imeisha na wao ndio mabingwa?

Ila Yanga imeandamwa na madeni.

Huku Yanga Princess wanadai, huku Bangala na Djuma Shabani nao wanadai.

Hawajakaa vizuri naye Lucy Eymael naye anawadai.

Nawashauri Yanga wakakope kausha damu walipe madeni yao
Juventus iliwahi mkuta hii si mara moja
 
Nani kasema media ilitatua swala la Feisali?

Nimesema mchango wa media katika kusaidia ishu ya Feisal kuwa solved.

Interview aliyofanya Clouds ilienda viral ikamfikia na Raisi ndio akaona ipo haja ya kuingilia kati.

Kwa maana hiyo Feisali angekaa kimya bila watu kujua kinachoendelea, ingewezekana vipi Rais kumsikia?
It's a wastage of time, kama madai yake yapo kisheria aende sehemu husika mzungu gani hana akili, mind you issue ya Feisal no siasa imefanyika na hio kitu imepanda mbegu mbaya sana huko mbele tukijaliwa uhai tutaona matunda yake
 
MABINGWA wa Ligi Kuu Bara na Kombe la ASFC, Yanga wanaweza kukumbana na rungu la kufungiwa kusajili katika madirisha matatu ya usajili ikiwa ni pamoja na kuondolewa msimu ujao kwenye michuano ya Kimataifa.

Uamuzi huo unaweza kufanywa muda wowote, kutokana na Yanga kushindwa kulipa kwa wakati deni la aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Luc Eymael.

Eymael aliiburuza Yanga kwa Shirikisho la Kimataifa la Soka Duniani (FIFA) kwa kosa la kuchelewa kumlipa madai yake miezi michache baada ya kibarua chake kuota nyasi, Septemba 2021.

Hata hivyo miamba hiyo ya soka la Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki ilikubali kumlipa kocha huyo kwa awamu.

Kwa mujibu wa notisi ya malipo ya Eymael, Yanga ilipaswa kumalizana naye ndani ya siku 45 huku kuanzia Juni 9 mwaka huu wakitakiwa kulipa na riba ya asilimia tano hadi juzi Ijumaa ambapo ilikuwa siku ya mwisho kumaliza deni la Dola 66,000 ambazo ni zaidi ya Sh. 157milioni.

Kocha huyo, ameliambia Mwanaspoti kuwa asilaumiwe kwa kile ambacho FIFA inaweza kufanya kufuatia Yanga kushindwa kukamilisha kile ambacho walikubaliana kuhusu malipo yake kwani hadi siku ya mwisho, juzi walikuwa wamemlipa nusu ya kiwango ambacho alitakiwa kupata.

"Nimekuwa nikifanya nao mawasiliano lakini naona wamekuwa kimya, kwa kuwa hili suala limefika kwenye mamlaka husika kwa hiyo tutaona kile ambacho wataamua, wanaweza pia kuingia kwenye adhabu ya kupokonywa pointi tisa,"

"Mwaka 2018 au 2017, Amazulu walikuwa na kesi kama hii, hawakulipa hivyo FIFA iliwalazimisha kulipa au kushuka daraja kabla ya msimu mpya kuanza, siku zote hakuna aliye juu ya sheria," alisema kocha huyo.

Kwa mujibu wa Eymael inamaana kuwa hadi siku ya mwisho ya malipo yote kufanywa, Yanga ilikuwa imemlipa Dola 33,000 (Sh78.8 milioni).

Yanga inaweza kuwa kwenye wakati mgumu zaidi kama FIFA itachukua maamuzi hayo kutokana na baadhi ya wachezaji wao muhimu kuwa mbioni kutimka akiwemo Fiston Mayele anayehusishwa na klabu mbalimbali kubwa ndani na nje ya Afrika kufuatia kuwa mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alitafutwa jana ili kutoa ufafanuzi wa jambo hilo, lakini simu yake haikupokelewa sawa na ilivyokuwa kwa Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo.

Chanzo: Mwanaspoti

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Yaan yanga kufungiwa clab bingwa kiss ms*nge mmoja tuu
 
It's a wastage of time, kama madai yake yapo kisheria aende sehemu husika mzungu gani hana akili, mind you issue ya Feisal no siasa imefanyika na hio kitu imepanda mbegu mbaya sana huko mbele tukijaliwa uhai tutaona matunda yake
Kwani hata sheria zenyewe mnazifuata?

Kama CAS tu wametoa amri mumlipe Lucy Eymael hela yake ndani ya siku 45 na mpaka saizi bado hamjamlipa unafikiri sheria pekee inatosha kuwafanya mheshimu Ethics za taasisi?
 
Ila huyu jamaa mbona kama walimvuruga sana maana kawakalia kooni. Hiki kisa halafu sikijui vizuri.
 
Kwani hata sheria zenyewe mnazifuata?

Kama CAS tu wametoa amri mumlipe Lucy Eymael hela yake ndani ya siku 45 na mpaka saizi bado hamjamlipa unafikiri sheria pekee inatosha kuwafanya mheshimu Ethics za taasisi?
Mimi una ni include kama nani? Kama CAS wametoa hukumu si asubiri utekelezaji
 
Mimi una ni include kama nani? Kama CAS wametoa hukumu si asubiri utekelezaji
Naku-include kama shabiki.

Hukumu ndio hiyo kulipa faini ambayo muda waliopangiwa umeisha na bado hela haijalipwa.
 

Attachments

  • ...Ah!....jpg
    ...Ah!....jpg
    26.3 KB · Views: 8
Yanga mpaka Sasa imeshasajili wawili Bado mmoja.
Wale mnao kerwa na hilo wakumbusheni CAF kuwa Yanga wanasajili wakati wamefungiwa.
 
Back
Top Bottom