Yanga hii inakusahaulisha hela ya sikukuu

Yanga hii inakusahaulisha hela ya sikukuu

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
224
Reaction score
236
Kila kitu na zama zake na huu ni wakati wa Yanga kuwa katika zama zake. Shukrani kwa GSM ambaye anasababisha mashabiki wa yanga tunasonga ugali tu mboga utaipata kwenye mechi yanga wanavyosakata kabumbu. Hizi pasi za Ntibanzoka zinasahaulisha watoto wasikudai nguo za sikukuu. Fei toto anavyozunguka uwanjani utadhani anatafuta mzingo na eneo la mstatili.

Kaze alichoamua sasahivi kaamua kutumia fumula ya fisi kwamba dont be choosy, you eat what you see. Kaze hataki kujua kama ulikula, ulishinda njaa, ulivimbiwa au una U.T.I anachokitaka yeye ni point tatu tu.Hiki kikombe kinampitia kila mtu hutaki au unataka. Deus Kaseke sasahivi anatukumbusha kuwa raha ya kwenda jandoni upate watu wazuri wa kukuongoza, What a player? .

Sitaki nizungumzie beki ya Yanga maana huo ukuta ni kama uliojengwa Mererani hakuna madini yatakayoweza kutoroshwa maana kuna mageti ya kutosha na kila geti unakutana na walinzi wa kutosha na unapovuka geti lingine unakutana na sura hizo hizo. Hapa ndio tunapoona kazi ya team work.

Yanga imeamua kuenzi falsafa za Mwl Nyerere kwenye ujamaa. Timu ya yanga ni ya kiujamaa mnalima kwa pamoja na mnavuna wote na kisha mnachokipata mnagawana kwa usawa na hiyo ndio maana ya timu ya wananchi.

Yacouba anatupa somo kuwa yaliyopota si ndwele tugange yajayo na wala Dar hakuja kushangaa vibao kata.
Hivi huyu Injinia Hersi bodi ya miss Tanzania wakimshirikisha miss world anatokea bongo, jamaa macho yake yanaona huenda siri yake anakula sana mchicha. Hii scout yake siyo ya kawaida huyu Tuisila atakuja apasue kifua cha mtu. Maana kuna mzee mmoja kidogo ateme nyongo[emoji23][emoji23].

Mlimwengu mimi ngoja niishie hapa maana hii Yanga imeanza kutibu watu nguvu za kiume haina haja ya kutumia vumbi tena.
#mlimwengumimi
#yangambeledaima
IMG_2028.jpg
 
abisa watani yaani rukhsa tangazeni ubingwa wala hakuna wa kukusumbueni mwaka huu ubingwa mali yenu.
 
Mi nawaomba tff wafanye mpango yanga icheze hata mechi 6 kwa wiki,hatuwezi kukaa kusubir mpk mwezi wa4/5 mbali sana
 
Watapita kama hawaoni wapo na fuso kwa sasa kurudi kesho kula maviporo yaliyochacha
 
Back
Top Bottom