Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ligi ina mechi 38, timu imeshakata pumzi tayari kama nimfuatilia mzuri wa mechi za kandambili!Usajili wetu ulikuwa wakuungaunga na jamaa walituita omba omba lakini Mungu mkubwa, timu inafanya vema! Na inshallah tutachukua kombe letu!
Kati ya hao wananchi mimi simoWanaitwa wa kimataifa,timu ya wananchi
Nani akujumuishe mkimbizi kama ww!Kati ya hao wananchi mimi simo
[emoji3]wakimbizi tunatambuanaga kumbeNani akujumuishe mkimbizi kama ww!
Aisee unachekesha kulinganisha yanga na mtibwa hali ukijua yanga amekosa ubingwa mwaka jana baada ya kuchukua mfululizo huku timu inayo kupa kiburi ilisubiri 5yrs.Sababu kubwa ni kuwa wanajua kikosi chao ni chembamba kwa maana hakina wachezaji wengi tegemezi, hivyo lazima round ya kwanza wakaze ili ikianza uchovu,majeruhi,mkataba,kocha hafai,mchawi fulani,marupurupu, n.k wawe at least kwenye big 5.
Mwendo wa Yanga ni mwendo wa mtibwa miaka yote ila hali huwa tete mzunguko wa pili. Mark my word.
NB. Morali ipo juu kwa sasa na wakipoteza mechi moja tu basi tayari lawama na nn, baadhi ya wachezaji kujiona ndio muhimu na kususia(Ajibu) baadhi ya mechi hadi kieleweke. Ww subiri mda uje utaona This is Tanzania. Only fans are sincere.
Yaani mwanangu kama ulikuwa hapa nyumbani vile. Kutwa kucha, fedha lukuki zinaenda kwa mlozi. Tuiue Yanga tu. Sasa, baada ya Yanga kufa, wewe mkia umefaidi nini?? Mpira wako mwisho jangwani?? Leteni basi kombe nje ya jangwani.Sisi Mikia mbumbumbu tunakesha tukiroga ili Yanga ifungwe lakini wapi sijui tunakwama wapi.
Yaani mwanangu kama ulikuwa hapa nyumbani vile. Kutwa kucha, fedha lukuki zinaenda kwa mlozi. Tuiue Yanga tu. Sasa, baada ya Yanga kufa, wewe mkia umefaidi nini?? Mpira wako mwisho jangwani?? Leteni basi kombe nje ya jangwani.
Nawadharau sana mikia. Pesa mnazosema mnazo ni za kuwanunua wachezaji wa Yanga na Azam tu au?? Tokeni nje mkatazame huko Ghana, Nigeria, Liberia na kwingineko kwenye mipira mbadili sura ya mpira bongo.
Kuna haja Serikali kujenga matawi ya milembe kila wilaya.Yanga wameamua wasiwe wapayukaji.
Wafadhili wapo na hata magoli ya Yanga ni quality sana, siyo mikia hata sijui wanafungaje.
Mikia wameamua kuhonga, mpira pale hakuna, they are too old.
Waala. Serekali iwapime mikojo mashabiki wote wa mikiatu baasiKuna haja Serikali kujenga matawi ya milembe kila wilaya.
Halafu hizo milembe ziwe na TV la sivyo kutakuwa hama watazamaji wa mechi za simba.Kuna haja Serikali kujenga matawi ya milembe kila wilaya.
Mbumbumbu wameshaanza kuleta umbumbumbu waohii timu ya magazetini tu juzi kmc wamewatoa jasho ngoja wacheze na azam labda wapaki tren ila sio ubingwa hata nafasi ya pili wasahau
Sentensi ya mwisho haina uhusiano na ulichoandika,ligi ndiyo kwanza iko mechi ya kumi bado mechi kama 28 tayari umeanza kucheka je kibao kikigeuka mwishoni na timu nyingine zikafanya vizuri kuliko yanga hapo nani atacheka mwishoniWalioidharau walikuwa wakiitizama kwa miwani ya mbao. Hawakujua kwamba asilimia kubwa ya wachezaji waliyoipa ubingwa miaka mitatu mfululizo bado wamebaki na timu. Ndiyo hawakuwa na morali. Lakini morali ni rahisi kuupandisha kama ilivyo rahisi kuushusha. Walidhani pesa pekee ndiyo inayoweza kupandisha ama kushusha morali. Waliamini kwamba Ngoma na Chirwa ni wachezaji wa kipekee dunia hii, na kuondoka kwao kungeiwachia Yanga pengo la milele. Waliamini kwamba timu ikishakuwa na wachezaji wenye majina makubwa, magoli yatajifunga yenyewe na kwa hivyo haingewezekana waliyoyaona kuwa ni majina madogo ndani ya Yanga yangeweza kufanya angalau robo ya ambayo yangefanywa na majina makubwa ya Simba, Azam na Singida. Hawakujua kwamba mwalimu ana nafasi kubwa katika ufanisi wa timu, na kwamba timu yenye uhaba wa pesa haiwezi kupata mwalimu mzuri. Waliamini kwamba mwalimu mzuri ni yule aliyepata kuzifundisha timu kubwa pekee, bila ya kujua kwamba ubora wa Mwalim hupimwa pia kwa alichokifanya kabla ya kupata jina. Waliamini kwamba kikosi kipana ni kile kilichosheheni majina makubwa, bila ya kujua kwamba zege haifanywi kwa nondo au saruji pekee bali lazima kokoto, mchanga na hata maji vipatikane. Kadhalika pilau haikamiliki kwa minofu ya nyama na mchele wa Mbeya pekee bali lazima na uzile, mdalasini, pilipili manga na hata zabibu ziwemo.
Ila hao wote walioko juu ya msimamo wa Ligi, na hasa washabiki wao, waweke akiba ya maneno maana sifa kubwa ya mpira ni matokeo yasiyotazamiwa. Nani angefikiria kwamba Real Madrid licha ya utajiri na majina yake makubwa ingepitia inakopita sasa? Nani alitarajia Borussia Dortmund kufanya vyema zaidi ya Bayern? Nani alitarajia Leicester ingetwaa ubingwa wa Uingereza mbele ya vigogo kama Arsenal, Man U, City na Chelsea? Ni mapema mno kuanza kutambiana na kukejeliana. Achekaye mwisho ndiye hucheka zaidi.
Jaalia mimi ni Yanga kama udhaniavyo kwa sababu tu maoni yangu yametokea kutowapendeza wapenzi wa Simba. Una uhakika gani kwamba mimi ni miongoni mwa walioanza kufurahia? Haiwezekani kwamba sentensi hiyo, kwa kujaalia mimi ni Yanga kama unavyohisi, inawaonya Yanga wenzangu wasianze kufurahia? Unapovuka barabara ya njia moja, angalia pande zote mbili kwanza. Usijihakikishie usalama kwa kuangalia upande mmoja tu, unaweza ukasombwa hata na mkokoteni unaotokea upande mwengine!Sentensi ya mwisho haina uhusiano na ulichoandika,ligi ndiyo kwanza iko mechi ya kumi bado mechi kama 28 tayari umeanza kucheka je kibao kikigeuka mwishoni na timu nyingine zikafanya vizuri kuliko yanga hapo nani atacheka mwishoni