Yanga hoi kwa Azam, yasambaratishwa magoli manne bila majibu

si kweli MAWAZO yako Azam alishapita alikuwa na point 4 zimamoto 3 JAMHURI 1 hivyo yanga na azam ilikuwa ni kutafuta Namba moja na kukamilisha ratiba acha kudanganya kuwa mmewàachia.
 
Nimeitazama match mwanzo mwisho. Nilikuwa sielewi sababu hasa ya wakenya kujitoa kwenye mashindano haya. Lakini kwa kitendo kilichofanywa jana, nakubaliana nao. Halafu pia mashindano ya mapinduzi cup yameshuka hadhi kabisa. Hayana umuhimu tena. Kama waganda wataendelea kushiriki mashindano haya, basi ni sababu ya njaa. Timu za Zbar zimepigana kutafuta kuingia nusu fainali halafu wengine wanapanga kuzitoa! Kweli kabisa timu zote za Zbar zinastahili kujitoa kwenye mashindano haya wawaachie timu pendwa. Aibu kubwa sana
 
Huna lolote umepigwa 4G unaanza kuneng'eneka, mbona uliposhinda 6 mbona hukueleza hayo?

Migomo FC bhana.!
 
ZIMAMOTO YAIPELEKA AZAM NUSU FAINALI MAPINDUZI

AZAM FC imefanikiwa kufuzu Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya Zimamoto kuifunga Jamhuri 2-0 jioni ya leo katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Matokeo haya yanafanya moja kwa moja Azam iungane na Yanga kwenda Nusu Fainali kutoka Kundi B, baada ya Zimamoto kumaliza na pointi tatu na Jamhuri pointi moja.
Katika mchezo huo, mabao ya Zimamoto yamefungwa na Hassan Ali dakika ya saba kwa kichwa, akimalizia krosi ya Rashid Ali na la pili dakika ya 59 mfungaji Ibrahim Ahmada baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Jamhuri.

Mchezo wa baadate usiku kati ya Azam na Yanga utakuwa tu wa kutafuta mshindi wa kwanza na wa pili wa kundi hilo, baada ya timu zote kufuzu mapema.
Hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inahitimishwa kesho kwa michezo miwili ya Kundi A, Simba na Jang'ombe Boys kuanzia Saa 10:00 jioni na URA na Taifa Jang'ombe utakaofuatia Saa 2:30 usiku.
Hadi sasa hakuna timu yenye uhakika wa Nusu Fainali katika Kundi hilo, ikiwa URA inaweza kufikisha pointi saba za Simba na Jang’ombe Boys na Taifa Jang’ombe wote wanaweza kumaliza na pointi tisa kila mmoja.

Source: Bin Zubeiry Sports Online
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Dah aisee.. Afadhali umejitokeza maana wenzako wamegoma kwenye jukwaa baada ya kupewa 4G

Mkuu wewe huna uwezo kuzifunga timu kubwa goli nyingi utasubiri sana
Unajua nini Kaabah , ukiona timu kubwa imeifunga timu nyingine kubwa mabao mengi basi hiyo si mechi iliyoamuliwa kwa uwezo wa timu bali kuna mtu kaotewa.

Kama umeicheki mechi ya jana, hususan lile bao la 4, utaona kabisa Yanga ilikuwa dhohfu wa hali. Yale waliofanya Azam ukiwaambia warudie wallah hawawezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…