Yanga huru

Balantanda

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2008
Posts
12,480
Reaction score
4,775
Kamati ya nidhamu ya TFF imewafungulia mabingwa wa soka wa Tanzania,Yanga kutoka katika adhabu iliyokuwa imepewa na TFF kufuatia Yanga kutopeleka timu uwanjani katika mchezo wa kombe la Kagame dhidi ya Simba..............Hata hivyo licha ya kufunguliwa Yanga imetozwa faini ya dola za kimarekani 20000(elfu ishirini) pamoja na viongozi wake kutakiwa kuomba radhi kwa TFF kwa kitendo kisichokuwa cha kiuanamichezo cha kutopeleka timu uwanjani..............Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF SAID HAMAD EL-MAAMRY amesema kwamba kamati yake imetengua uamuzi huo wa TFF kwa vile hakuna kifungu kinachoeleza adhabu ya miaka miwili(02) kwa timu itakayogoma kuingia uwanjani.Kwa hali hiyo TFF ilitakiwa kutumia kifungu cha adhabu cha FIFA ambacho ni adhabu hiyo (ya dola 20000) iliyotlewa na kamati ya nidhamu ya TFF
 
Kamati hiyo inadaiwa imeona kuwa TFF haikupaswa kuiadhibu Yanga kutokana na kuwa mwenyeji tu wa michuano hiyo inayosimamiwa na Baraza la soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).................Hata hivyo akina El Ma-amry walijadili rufaa hiyo licha ya pingamizi kubwa toka kwa wawakilishi wa TFF katika kikao hicho Katibu Mkuu Fredrick M wakalebela na Mkurugenzi wa Ufundi Sunday Kayuni waliojenga hoja kuwa kamati hiyo haina mamlaka ya kujadili rufaa hiyo................Hali hiyo ilisababisha ubishani mkali ulioanza saa 10:10 jioni hadi 12:17 jioni nabaadae kamati ilikaa na kumaliza kikao chake kwenye saa moja na nusu usiku (www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/08/120320.html
 
Sasa itakuwaje wakati tunaambiwa hata CAF vilevile waifungia Yanga?
 
Ukitaka kudhitibisha mpira wa bongo 'utumbo' mtupu embu sikia ya hapo juu.....yaani hata TFF hawajui sheria zao wenyewe walizotunga?... #$%@&...
Kwa wengine tulijua tu..kwamba ile adhabu ilikuwa kama 'dua ya kuku' vile, yaani waifungie Yanga/Simba wakale wapi?

Scrap....scrap...scrap...scrap!!
 
Sasa itakuwaje wakati tunaambiwa hata CAF vilevile waifungia Yanga?

achana na magazeti ya udaku hayo.
yanga ilianzishwa 1935 hivyo hao kina tenga na mwakalebela sisi tunawaona machizi tu kwa sababu yanga ilikuwepo kabla ya wao kuzaliwa so hawawezi kukurupuka tu na kuifungia yanga.
 
na ushindi ule tulioupata yanga katika adhabu dhidi ya TFF ni salaam kwa Musonye na wajaluo wenzake wasiofahamu nini maana ya tohara....naomba kuwasilisha salaam
 
unaongelea nini, kwanini usitoe huo upuuzi wako, mimi naomaba TFF waliangalie upya tena hili swala kama hawana sheria za kuwa zibiti wahawa wanao vamia soka wazitunge ili ikitokea tena kiongozi akatoa uamzi walioutoa akina madega na wenzake wafutwe kabisa yaani wasijihusishe na soka tena.....
 

Unazungumzia upuuzi upi mkuu????????.....maana yameongelewa mengi sasa sijui ni upuuzi upi unataka uondolewe.....kuwa specific mkuu
 
achana na magazeti ya udaku hayo.
yanga ilianzishwa 1935 hivyo hao kina tenga na mwakalebela sisi tunawaona machizi tu kwa sababu yanga ilikuwepo kabla ya wao kuzaliwa so hawawezi kukurupuka tu na kuifungia yanga.
Haya mambo hayataisha kirahisi hivyo; angalia hii ya leo kwenye Majira

MAJIRA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…