Yanga ijenge uwanja wake

Yanga ijenge uwanja wake

fimboyaasali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
8,617
Reaction score
8,244
Nawashauri hawa viongozi wetu wa Yanga wajitahidi juu chini wajenge uwanja wetu, ni uwekezaji mzuri sana.

Jambo hili walipe kipaumbele.
 
Yanga na Simba haziwezi kujenga uwanja mdogo kama wa Azam Complex wa watu 6,000, inabidi wajenge uwanja wa kuingiza mashabiki kama 20,000-30,000. Kumaintain uwanja wa size hiyo kwa maana ya usafi na ulinzi ambavyo inabidi vifanyike hata siku zisizo na mechi, pamoja na matengenezo ya mara kwa mara si jambo dogo. Inawezekana lakini inabidi kujipanga hasa.

Gharama za kumiliki kiwanja ukilinganisha na urahisi uliopo wa kutumia uwanja wa Mkapa inafanya klabu hizi zione ugumu kubeba jukumu hili.
 
Naunga mkono hoja.. Watu wanaongea nadharia tu
 
Huyu naye Asikilizwe....Yanga Wanatakiwa Wajenge Kama Simba Sports club Kule 'Mo Arena'..!

Ukibisha Unapigwa.!!
 
Yanga ina mashabiki zaidi ya 30,000,000 kila shabiki akitoa 10,000 hiyo ni Trillion 3, tuainunua Simba tunaibadili inakua timu ya cricket
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Yanga na Simba haziwezi kujenga uwanja mdogo kama wa Azam Complex wa watu 6,000, inabidi wajenge uwanja wa kuingiza mashabiki kama 20,000-30,000. Kumaintain uwanja wa size hiyo kwa maana ya usafi na ulinzi ambavyo inabidi vifanyike hata siku zisizo na mechi, pamoja na matengenezo ya mara kwa mara si jambo dogo. Inawezekana lakini inabidi kujipanga hasa.

Gharama za kumiliki kiwanja ukilinganisha na urahisi uliopo wa kutumia uwanja wa Mkapa inafanya klabu hizi zione ugumu kubeba jukumu hili.
Kwanini wajenge 20,000, wastani wa mashabiki kwa mechi moja ni 6,000 mpaka 7,000 ukiachana na mechi za mahasimu. By the way kwenye ujenzi structure inaweza kujengwa na kuweka provision ya kuextend miaka ya baadae, ni mipango tu
 
Mpaka leo hata sielewi ule mradi wa Kigamboni ulipoishia.
Yaani katika hili, siwezi kufungamana na viongozi wa Yanga wasiosimamia ahadi zao.

Ni vizuri wakawa na mpango makakati wa kujenga uwanja wa mazoezi pamoja na mechi! Lakini pia hostel kwa ajili ya wachezaji wake.
 
Yanga ina mashabiki zaidi ya 30,000,000 kila shabiki akitoa 10,000 hiyo ni Trillion 3, tuainunua Simba tunaibadili inakua timu ya cricket
Hesabu za motivational speakers hizi wanakwambia ukalime matikiti uwe bilionea.
 
Kwanini wajenge 20,000, wastani wa mashabiki kwa mechi moja ni 6,000 mpaka 7,000 ukiachana na mechi za mahasimu. By the way kwenye ujenzi structure inaweza kujengwa na kuweka provision ya kuextend miaka ya baadae, ni mipango tu
Wakijenga wa watu 20,000-30,000 uwanja unaweza kutumika hata katika mechi kubwa za ligi au kimataifa ukiachana na debi. Najua utasema mechi hizo ziende kwa Mkapa kwa sababu una uwezo wa kubeba zaidi ila nitakwambia kwa nini watumie viwanja vyao hata katika mechi hizo.

Uwanja ukiwa mdogo kulinganisha na mahitaji ya mechi hizo kubwa, klabu zitaweza kuanza taratibu za kuuza tiketi mapema sana hata mwanzoni mwa msimu ili watu wazinunue mapema. Hii itazipa klabu uhakika wa mapato mapema maana itafika wakati tiketi zinagombaniwa na wataweza kutumia mapato hayo ya mapema kwa shughuli za klabu. Hata bei za tiketi zitawekwa kulingana na ukubwa wa mechi na kwa sababu mahitaji ni makubwa kuliko uwezo wa uwanja hii pia itaziongezea vilabu mapato.

Kuhusu upanuzi, pale Azam Complex wakitaka kupanua uwezo wa uwanja, itabidi wabomoe majukwaa yote yale ya mzunguko. Kujenga uwanja siyo sawa na kujenga nyumba.
 
Gharama ya kujenga uwanja na kuhudumia ni kubwa sana.

Mi siwezi kushauri zijiingize kwenye hiyo hesabu kwa mkapa panatosha

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Hata wakijenga uwanja kuna baadhi ya mechi hazitochezwa katika huo uwanja
 
Wakijenga uwanja utopolo mimi naenda kuishi zimbabwe
 
Back
Top Bottom