Yanga ijenge uwanja wake

Yanga ijenge uwanja wake

Wakijenga wa watu 20,000-30,000 uwanja unaweza kutumika hata katika mechi kubwa za ligi au kimataifa ukiachana na debi. Najua utasema mechi hizo ziende kwa Mkapa kwa sababu una uwezo wa kubeba zaidi ila nitakwambia kwa nini watumie viwanja vyao hata katika mechi hizo.

Uwanja ukiwa mdogo kulinganisha na mahitaji ya mechi hizo kubwa, klabu zitaweza kuanza taratibu za kuuza tiketi mapema sana hata mwanzoni mwa msimu ili watu wazinunue mapema. Hii itazipa klabu uhakika wa mapato mapema maana itafika wakati tiketi zinagombaniwa na wataweza kutumia mapato hayo ya mapema kwa shughuli za klabu. Hata bei za tiketi zitawekwa kulingana na ukubwa wa mechi na kwa sababu mahitaji ni makubwa kuliko uwezo wa uwanja hii pia itaziongezea vilabu mapato.

Kuhusu upanuzi, pale Azam Complex wakitaka kupanua uwezo wa uwanja, itabidi wabomoe majukwaa yote yale ya mzunguko. Kujenga uwanja siyo sawa na kujenga nyumba.
ni kupata tu macontractor wazuri; anfield, camp nou wametanua vizuri tu bila kuhama uwanja hivi karibuni
 
Back
Top Bottom