Yanga iko mbioni kumtambulisha mshambuliaji Kenedy Musonda

Yanga iko mbioni kumtambulisha mshambuliaji Kenedy Musonda

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
YANGA wakati wowote kutoka leo itamtambulisha mshambuliaji Kennedy Musonda akitokea Power Dynamos ya Zambia, lakini jeuri ya fedha ndefu ndiyo inamshusha Mzambia huyo huku kocha mmoja mkubwa akisema wananchi wamelamba dume haswa.

Taarifa kutoka Zambia ni kwamba Musona ambaye amesajiliwa na Yanga amepewa dili la maana na timu hiyo ya Jangwani na sasa atatakiwa kufanya kazi haswa ili kuwapa imani mashabiki wa timu hiyo.

Dynamos imechukua fedha nzuri katika dili hilo kiasi kisichopungua sh 150 milioni kutoka kwa Yanga ambao wamenunua mkataba wa staa huyo uliokuwa umebaki.

Mbali na klabu hiyo pia Musona mwenyewe amechukua kiasi kama hicho ili kusaini dili la miaka miwili na Yanga huku mshahara wake ukiwa 11 milioni kwa mwezi akiwa kati ya wachezaji wanaolipwa ghali zaidi kwenye Ligi Kuu Bara kwa sasa.

Staa huyo mwenye miaka 29, ambaye anatajwa kuwa alitua nchini jana na kufichwa kwenye hoteli moja ya jiji la Dar es Salaam.

akisubiri kutambulishwa na timu hiyo ametoka kwenye timu yake akiwa ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Zambia, baada ya hadi sasa kuwa ameshafunga mabao 11.

Mshambuliaji huyo ambaye aidha watacheza pamoja au mmoja ataanzia nje kati yake na Fiston Mayele mwenye mabao 14 kwenye ligi msimu huu, aliwahi pia kuzichezea Lusaka Dynamos, Zanaco na Green Eagles kwa mafanikio makubwa.

Msikie Lwandamina

Kocha wa zamani wa Yanga na Azam FC George Lwandamina 'Chicken' ameliambia Mwanaspoti kwa simu kuwa Yanga kama wamekamilisha dili la Musonda wamepata mtu wa kazi ambaye sio rahisi kuzuiwa na beki mmoja.

Lwandamina alisema Musona ni mshambuliaji mwenye nguvu anayejua kupambana na mabeki wa aina yoyote na kwamba atawasaidia Yanga.

"Nimeona hapa hizo taarifa tangu jana, bila shaka ni usajili mzuri kwa Yanga, huyo ni mshambuliaji mwenye nguvu sio nzuri na rahisi kubaki na beki mmoja kisha akafanikiwa kirahisi kumzuia,"alisema Lwandamina ambaye amelamba dili nono kurejea Zesco ya Zambia.

"Anajua kufunga pia nguvu zake na uwezo wa kumiliki mpira na mbio zake nadhani kwa hapo Tanzania kama akianza vyema tu atafanya vizuri na kuisaidia Yanga."

SOURCE: Mwananchi
 
Kwa hiyo Simba wamelambishwa Mavi? Haya mambo ya kulamba lamba sijui Yanga wamelamba nini achana nayo.

Kiufupi mimi ni shabiki ya Simba Sport japo tunapitia kipindi kigumu lakini jasiri haachi asili Mtani, tutaendelea kuwapumulia visogoni mkiwa kileleni
 
Mashabiki wa simba kila siku mnnamuota Manzoki!! Ambaye hata hamjui kama atasajiliwa lini na Mwamedi.
 
Mashabiki wa simba kila siku mnnamuota Manzoki!! Ambaye hata hamjui kama atasajiliwa lini na Mwamedi.
Dada sisi hatuna hz story za kijiweni bali tunapanga mipango ya kuvuka group stage CAFCL na ma forwad wetu si wengne ni Bocco+kibu+kyombo+phiri ko kaa kwa kutulia punguza mihemko
 
Kwa hiyo Simba wamelambishwa Mavi? Haya mambo ya kulamba lamba sijui Yanga wamelamba nini achana nayo.

Kiufupi mimi ni shabiki ya Simba Sport japo tunapitia kipindi kigumu lakini jasiri haachi asili Mtani, tutaendelea kuwapumulia visogoni mkiwa kileleni
Unapitia wewe kipindi kigumu. Sisi lialia tunaiombea Simba yetu mwisho mwa msimu tubebe makombe yote na inshaaaaalah tutayabeba!!
 
Dada sisi hatuna hz story za kijiweni bali tunapanga mipango ya kuvuka group stage CAFCL na ma forwad wetu si wengne ni Bocco+kibu+kyombo+phiri ko kaa kwa kutulia punguza mihemko
Una udumavu wa akili bila shaka. Maana unaweza kukuta siku nyingine, unamuita baba yako 'mama'.
 
Back
Top Bottom