Yanga ilishinda kwa uwezo wa mchezaji Mmoja Mmoja

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Jana tumeshuhudia Gemu ya Yanga na Mbeya city ahaa kabla ya kuendelea nina jezi za Yanga Ndani najua ushaelewa namaanisha nini.

Dakika 90 zote zilikua za jasho damu na machozi hasa kwa upande wa Yanga ukitegemea wao ndio walikuwa wenyeji na Pressure ya mashabiki wakitaka ushindi.

Uhalisia Mbeya city tangu aje Amri Said kama kocha wamekuwa na Tabia ya kuikamia sana Yanga same same na Jana Mbeya city waliikamia sana Yanga kama walivyofanya ndg zao prison.

Kwenye Pointi ya Msingi.Ukiangalia gemu ya Jana Matokeo yaliamuliwa na uwezo binafsi wa wachezaji Yanga kwa sasa imesinya Wachezaji wazuri wenye majina na uhalisia wana viwango vizuri tu ila kila mchezaji anacheza kivyake hakuna mfumo wa wazi ukiangalia Tuisila anatumia uwezo binafsi anataka kupiga chenga uwanja mzima,Likewise kwa Sarpong,Yacouba...nk

Angalau Mukoko,Nondo,Feisal wanacheza kitimu ni mapema sana kulaumu benchi la ufundi kwani wamekaa na timu kwa muda mfupi sana nawapa angalau Gemu 5 ndio ntaweza kutoa Tathmini Yangu Juu yao.makocha bado wana kazi kubwa sana ya kuunganisha timu ili timu iweze kucheza kimfumo na sio mchezaji Mmoja mmoja.

Narudia tena wachezaji ni Grade A na B Natumai makocha hawatakua na kazi kubwa sana na kuanza kufundisha kutuliza mpira,kutoa pasi ishu kubwa ni Muunganiko wa Timu tu.

Nategemea watu waanze kula dozi kubwa kubwa kutoka kwa Chama langu Yanga.
 
Yanga wameenda kutafuta akina Yikpe, Molinga na PS machine waliochangamka

Yanga ni mbovu ila inawafariji tu saivi
 
Wewe kweli ni mwenzetu. Maana ma mbumbumbu humu yana kawaida ya kujivisha joho na kujifanya nao ni wenzetu, kwa lengo tu la kutaka kutusanifu.

Ukweli mwaka huu tuna timu nzuri ukilinganisha na msimu uliopita. Ni suala tu la muda. Wachezaji wakishazoeana, hakika timu yetu itatisha sana.
 
Back
Top Bottom