Yanga imepangwa kundi D katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

boy lanugo

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2015
Posts
290
Reaction score
272
Katika makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga SC ya Tanzania imepangwa katika Kundi D pamoja na na Rayon Sports (Rwanda), U.S.M Alger (Algeria) na Gor Mahia (Kenya).

Yanga ilifuzu hatua ya makundi baada ya kuiondoa Welatya Dicha ya Ethiopia kwa magoli 2-1.

Kwa timu hizi ninahakika yanga ikiamua hatua ya robo fainali inawahusu..

======

Wawakilishi pekee wa Tanzania timu ya Yanga imepangwa kundi D katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika safari hii itakutana na timu mbili ambazo zipo katika ukanda wa CECAFA pamoja na USM Alger kutoka nchini Algeria.

Kila timu kwenye kundi itacheza mechi 6 ikiwa mechi 3 nyumbani na mechi 3 ugenini Mechi za makundi ya Caf Confederation cup zitachezwa
Mechi ya kwanza May 4-6
Mechi ya Pili May 15-16
Mechi ya tatu July 17-18
Mechi ya nne July 27-29
Mechi ya tano August 17-19
Mechi ya sita August 28-29

KUNDI A
1-Asec Mimosas (Ivory Coast)
2-Raja Casablanca (Morocco)
3-AS Vita Club (DRC Congo)
4-Aduana Stars (Ghana)

KUNDI B
1-RS Berkane (Morocco)
2-Al Masry (Egypy)
3-UD Songo (Mozambique)
4-Al Hilal (Sudan)

KUNDI C
1-Enyimba (Nigeria)
2-Williamsville (Ivory Coast)
3-CARA brazavile (Congo)
4-Djoliba (Mali)

KUNDI D
1-USM Alger (Algeria)
2-Yanga Sc (Tanzania)
3-Rayon Sports (Rwanda)
4-Gor Mahia (Kenya)
 
Aisee kucheza na watu mnafahamiana ni kazi sana... Hapa Yanga afanye usajili mzuri kama kuna option hata striker na kiungo
 
aisee mpk mwezi wa nane? ligi itaanza msimu ujao yanga bado wapo kwenye hya mashindano!
 
Timu za waarabu katika ubora wao. Huwa nawakubali mno hawa viumbe..hawanaga utani uwanjani. Yanga vichapo vinawahusu 😛😛😛
 
Hapa ni kuweka mikakati sawa tu. tufanye usajili wa maana vinginevyo tutapoteana kwa kudhani kundi ni jepesi.
 
Angelikuwa kocha hvp ililuwa robo fainali bila utata
 
Inatakiwa maandalizi zaidi Mtani ili zipatikane sababu hazina Ushindani sana kama USM Alger.
Hapo ni kujiandaa vyema na hakika kwa kundi lenu mnafuzu nyie na USM Alger....

Maana huyo muarabu ni habari nyingine....
 
Hapo ni kujiandaa vyema na hakika kwa kundi lenu mnafuzu nyie na USM Alger....

Maana huyo muarabu ni habari nyingine....
Kweli kabisa na mimi nasisitizia maandalizi tu bila hivyo hizo Gormahia na Rayon Sport pia zinaweza tutoa kijasho.
 
Kweli kabisa na mimi nasisitizia maandalizi tu bila hivyo hizo Gormahia na Rayon Sport pia zinaweza tutoa kijasho.
Kidogo rayon sport mtani... but siku zote wanasema ni bora kuomba kheri kuliko shari....

So lets hope for the best mtani...
 
Yanga wakizichanga vizuri basi Hilo kundi atapita Yanga na USM alger. Akimpiga alger kwao basi watakuwa wameanza mbio vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…