Yanga imerudi nyuma hatua kumi

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Naangalia mechi ya Yanga dhidi ya KMC dah kwakweli timu ya Yanga inatia hadi aibu yaani wachezaji kupiga pass hawawezi, kukontroo mpira hawawezi, kutengeneza nafasi hawawezi wanaishia kubebwa na mwamuzi tu kwa mchezo wa kujiangusha angusha.

Hivi kweli ndio akili ya viongozi wa Yanga ndio akili zenu zilipoishia hapo? Unafuka benchi la ufundi halafu hakuna cha maana.
 
Tatizo la utopolo ni wanachama wake wengi akili ndogo sana.Sijui kuna uhusiano gani kati ya watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri na rangi za kijani na njano!

Yaani wanaamini wachezaji wao ni wa kiwango cha juu mno,ila TFF tu ndio inawahujumu.

Kesho utasikia analaumiwa Rais wa TFF
 
Mnafukuza kocha katikati ya msimu mnajidai Barcelona, badala msubiri wachezaji majeruhi wapone waungane na timu nyie mkasubiri wapone then mkafukuza kocha, tulieni sasa sindano ziingie.
 
Sijui tutajifichia wapi Sasa

Ushauri tu kama yanga itafuzu klabu bingwa au shirikisho tff waikatalie isishiriki hadi pale itakapo kuwa na kikosi imara

Ikiruhusiwa itaenda kutia aibu huko duniani
 
Unaakili Sana jamaa

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Utopolo wasipoacha Wenda wazimu wao wa kuabudu shirk na kulalama kila mahali hata pasipostahili watapata tabu sana maisha yao yote.
 
Mnafukuza kocha katikati ya msimu mnajidai Barcelona, badala msubiri wachezaji majeruhi wapone waungane na timu nyie mkasubiri wapone then mkafukuza kocha, tulieni sasa sindano ziingie.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Unawasaidiaje sasa, maana maneno matupu hayawasaidii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenzao wanawekeza kwenye benchi la ufundi na wachezaji bora wao wamekalia kuwekeza kwa waandishi wa habari na marefarii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…