Yanga inahitaji kujengwa upya

Yanga inahitaji kujengwa upya

Unknown2

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2016
Posts
2,352
Reaction score
5,055
Salamu wakuu!

Kwa wale mnaofuatilia michezo mtakubaliana na mimi kuhusu mambo haya:
1. Wachezaji muhimu wote wamechoka hali inayosababishwa na umri wao kuwatupa mkono ama kutojitambua. Hapa kuna Donald Ngoma, Hamis Tambwe, Thaban Scara Kamusoko na Nadir Haroub.

2. Utovu wa nidhamu uliopitiliza! Hapa tunamkuta Ngoma na Obrey Chirwa.

3. Ukata unaoiandama timu ambao binafsi naona unasababishwa na ama uzembe wa viongozi au kumuamini sana Yusuphali Manji.

4. Kocha kushindwa kuzichanga karata zake kulingana na wachezaji alionao ambapo binafsi naamini hakuwahi kusajili yeye mwenyewe bali huletewa wachezaji wa gharama nafuu baada ya kutoa mapendekezo.

Kwa sababu hizo nne, Yanga inahitaji mabadiliko makubwa ya kikosi na kiuchumi. Msimu huu ni wazi kabisa kwamba hakuna kombe litakalotua Jangwani na ni bora wanachama na wapenzi kujiandaa kisaikolojia ili kuepusha ugomvi usio na tija ndani ya klabu hapo badae.
 
Na mabadiliko yenyewe utaskia wameenda kupiga magoti kwa manji.
 
Nimeshakuja Babu.

Kweli sie Wanajangwani tunahitaji mabadiliko ya hali ya juu.

Msisahau na hili tatizo jingine...
upload_2018-1-18_20-28-50.jpeg
 
Wakimataifa wanahitaji ujenzi....!
Mmezisahau wapi MBAO za kujengea ?
 
Back
Top Bottom