Yanga inahitaji mabadiliko ya haraka kwenye benchi lake la ufundi

Anselm

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2010
Posts
1,710
Reaction score
291
Inajulikana kuwa Noel Mwandila amekuwa ni msaidizi wa George Lwandamina kwa muda mrefu,na iliwahi kusemwa Chicken hupenda kufanya naye jazi...Lwandamina ameshaondoka na inasemekana amerudi kwenye team yake ya zamani(Zesco),hiki Kijamaa kinasubiri nini sasa?,peleka yeye kwa Boss wake,shusha Nsajigwa akafundishe team B,kamilisha upatikanaji wa vibali vya Mwinyi Zahera ili aweze kuanza kazi mara 1 huku mkimtafutia msaidizi kwa haraka.
Kama kuna nafasi ya kusajiri katika hatua hii ya Makundi,Yanga inahitaji Striker mwingine, kama ni Mzawa Adam Salamba wa Lipuli anaweza kuongeza kitu kwa gharama ya kawaida I guess.
Mwanachama mtiifu.
 
Adam Salamba namkubali sana, dogo anajituma mno kwa sasa.
 
ha ha ha ha unamsajili salamba akakusaidie kupata matokeo kwa waalgeria ?
 
Adam Salamba namkubali sana, dogo anajituma mno kwa sasa.

hyu salamba namfananisha na bahanuzi anapata nafasi kumi anafunga goli moja...

yanga km kweli wanatka kumsajili wasikurupuke!! wajipe muda kumfatilia kujiridhisha na perfomance yake na sio kwa ajili kamfunga simba tu!!!
 

Yanga ina matatizo makubwa sana, lakini kubwa kuliko yote ni lile la udhaifu wa uongozi au top leadership...Wengi na hasa viongozi wale wa juu kiutendaji hawana sifa za kuchukua nafasi ya utendaji..Kwa mfano hivi kweli mtendaji mkuu wa klabu anachukuliwa kocha kwa kuwa tu eti amepigiwa debe kwa 'Manji'??? Is Yanga serious??? Yaani professionals wa nafasi za kiutendaji tena ambao ni Yanga wapo lakini eti mtu anapigiwa debe hata kuchukua nafasi kubwa ya kiutendaji baadala ya ukocha...halafu wapiga debe hao ambao ni makomandoo baadhi yao wanaiyumbisha klabu...halafu viongozi wengi kwenye kamati ya utendaji hawana sifa za uongozi au utendaji ukiacha sifa zao kubwa za kutaka umaarufu kwenye vyombo vya habari...

Hivi sasa wachezaji wa Yanga tunaelezwa hawajalipwa mishahara miezi mitatu...you can just imagine...Of course kosa kubwa lilikuwa ni lile la kumtegemea mtu mmoja kwa kila kitu...watu makini walijua tu kwamba huyo akiondoka Yanga itayumba...mishahara ya wachezaji ilikuwa inflated ambapo hakuna kiongozi mwingine anayeweza kuja kuimudu hiyo mishahara....halafu wachezaji hawafundwi kuhusu nidhamu mchezoni...wewe mchezaji una kadi moja ya njano but, yet, unaendelea kufanya faulo za kijinga, ni refa gani ataacha kukupa kadi ya pili ya njano...of course wako wachezaji baadhi hawastahili kabisa kuvaa jezi hiyo ya njano na kijanina nyeusi...kiwango chao ni cha chini mno, ila walipata nafasi kuichezea Yanga kutokana na 'njama' za madalali...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…