Yanga inatakiwa iache kushiriki kwa kukariri

Efendi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
314
Reaction score
438
Na Ally Mayai Tembele

Niliwahi kuandika Yanga inajidanganya yenyewe na kuishi kwa kivuli cha timu kubwa na kudhani labda dunia imesimama kumbe dunia inakimbia kwa kasi mno.

Nilisema Yanga imedumaa na Siku ikija kushtuka na kutaka kwenda sambamba na dunia itakuta tayari Simba imeliteka soko lote la Uchumi wa soka nchini.
Nilitoa mfano wa Juventus, Porto, Buyen Munich, Mazembe, Gor na Horoya kwamba timu hizi tayari zimejimilikisha Uchumi wa soka wa nchi zao. Leo hakuna mchezaji wa Kijerumani asiyetamani kuchezea Buyern. Au mchezaji anayezaliwa Italy ndoto yake kuu ni kucheza Juventus. Na tunakoelekea na Tanzania hali ndiko inakoelekea. Simba inajimilikisha kwa kasi ya ajabu uchumi wa soka.
Yanga wamebaki kujivunia juzi na jana na sio leo na kibaya zaidi sioni kesho yao.
Kama Kuna kosa kubwa kuliko yote linafanyika ni pale wanapobeza mafanikio ya Simba na kuwaponda mwekezaji wa Muhamed Dewj. Wamekuwa wakitafuta mapungufu machache yaliyopo Simba na kuyafanya ndio agenda yao. Wamesahau kabisa kuitazama timu yao na mkwamo uliopo wameamua kuitukuza Simba na kuitaja aidha kwa mapungufu au kuwabeza Kama watani. Wanasahau hapa wao wenyewe ndio wanaikuza brand ya Simba na kuifanya kutajwa mno midomoni kila siku.

Leo Yanga hawana hata Jambo Moja wanaloweza kupambana na Simba aidha ndani au nje ya Uwanja. Wamezidiwa kila udara na itawachukua muda mrefu mno kufikia Simba ilipo Sasa.
Yanga hawajakubali bado kubadilisha mfumo wao wa uendeshaji wa timu kutoka wa kizamani na wa kiholela kuja kwenye mfumo wa kisasa na hii inasababishwa na walaghai tena wezi wa jasho la wachezaji kuwahadaa ni timu ya wananchi na wasikubali mwekezaji kwa kuwa timu itakuwa si Mali yao Tena. Huu ndio uongo uliotukuka wanaoutumia walaghai kuendelea kujinufaisha kupitia klabu hii.
Embu tujiulize nyie wapenzi na mashabiki wa Yanga lini mlinunuliwa hata soda na klabu zaidi ya nyie kuchangishwa? Sasa hicho mnachoaminishwa mtakipoteza ni kipi? Wanaoogopa kupoteza ni wale akina fulani ambao maisha yao yanategemea timu kuendelea kuishi mjini. Na hawa huwa hawachangii zaidi ya kuwa mstari wa mbele kuhamasisha ili wazizungukie mlango wa nyuma wakaziibe. Sisi tunaochanga Wala hatuna Cha kupoteza

Nahisi kwenye miaka ya sitini ni kweli mashabiki wa Yanga labda walikuwa wengi kuliko wa Simba na mkabweteka na mkasahau watu wanazaliwa na kufa. Nimebahatika kwenda karibu viwanja vyote vya soka nchini. Nawahakikishia kwa sasa Simba Ina mashabiki wengi kuliko timu zote nchini.
ENDELEENI KULALA MKIAMKA TAYARI JUA LITAKUWA LINAZAMA.
 
Maneno ya kweli yaliyosemwa na mchezaji wa zamani wa Yanga,mwanachama, na mchambuzi makini wa soka nchini. Bakini kuendekeza historia huku Simba ikisonga mbele kisasa. Na uzuri hakuna anayeweza kudai aliyeandika makala haya hapendi Yanga kwani anajulikana.
 
safi
 
Ally mayai binafsi kwangu ni moja ya wachambuzi wanaoijua kazi yao,huyo ni shabiki na mwanachama wa Yanga lakini huwezi jua yupo upande gani anapofanya uchambuzi,hilo andiko lake limeeleza kila kitu
 
Vyura hawa hawajitambui kabisa!! mimi ngajapo karibia thread nyingi nimeongelea hili jambo sijui kama wananielewa kuhusu kuwaamnisha mashabiki kwamba hii ni timu ya ''wananchi'' na inatakiwa idhaminiwe na wananchi wenyewe halafu mechi ikifika wanaanza kutembeza mabakuli uwanjani pasipo na utaratibu wa mfumo wa kifedha halafu wananchi hawa wanashangilia kama mazuzu then hawajui hata hela walizokunsanya ni kiasi gani na nani aliyekusanya (maana wanakuwa wengi tu wanazungusha mabakuli uwanjani) na kama hela zote zimeingizwa kwenye mfumo sahihi wa taratibu za kifedha au zimetumikaje??? halafu baadae wakisikia akina Yondani hawapo kambini kwa sababu ya kutolipwa fedha zao wanabaki kushangaa eti mbona tumechangia sana.. ukiwauliza mmechangia kiasi gani?? wanakosa jibu!!
 
Ukweli mtupu lakini wale wajinga waliobadilishiwa mpaka jina ili na wao waonekane wana share kwenye timu kwa kuitwa wananchi wakati hawajawahi kununuliwa hata andazi na timu wataupinga ukweli huu... eti tukimpa mwekezaji timu tutaikosa mijinga kabisa na ndo mana manji kawakimbia. Timu inaendeshwa kizamani kabisa. Mimi ni simba wa kutupwa lakini sipendi kuona watani wanapitia magumu kwani kwa sasa upinzani umekwisha, na ndio sababu tukikutana nao ushindi wao droo
 
Mamluki lingine hili la Mikia halijua kwamba Mikia inaendeshwa na mmoja kama ilivyokuwa Yanga ya Manji
 
Mamluki lingine hili la Mikia halijua kwamba Mikia inaendeshwa na mmoja kama ilivyokuwa Yanga ya Manji
Huoni aibu wewe kumuita Ali Mayai mamluki???Huwezi kufikia hata kidogo alichoifanyia Yanga.Sidhani hata kama wewe ni mwanachama wa Yanga.Tabu ya wapenzi maandazi kama wewe mkiambiwa ukweli kwenye hizi timu mbili mnakimblia kumuita aliyesema ukweli mamluki badala ya kujibu hoja kwa hoja.
 
Ally anaonekana kuwa na point moja muhimu. Hakuna ujinga unaozidi ule wa kila siku Mikia wakifanya jambo Yanga nao wanajaribu kuonyesha kuwaliwahi kufanya enzi zile. Mbumbumbu akijaza uwanja Yanga wanalilia haki ya wao kujaza uwanja enzi za Manji, what for? Mbumbumbu wakifurahia kupanda ndege Yanga nao wanadai walizipanda mpaka wakachoka!!

Sehemu moja muhimu nitakayompinga Ally ni kwenye kuteka soko. Ukiangalia kwa makini soka la Tanzania linavuma na upepo. Kilichopo Simba kwa sasa ni kile kile kilichopata kuwapo isipokuwa kimeboreshwa kiasi. Wakati Simba inakwenda kwa ya mtu mmoja, siku akisusa kama ilivyotaka kutokea mpaka waziri na rais wakaingilia, mfumo mzima wa club utaanguka. Kwa maoni yangu si vema timu ikaendeshwa kwa kivuli cha wanasiasa ambao hubadilika mara kwa mara. Ingawa hoja ya Mwakyembe kuhusu kuwa na wawekezaji zaidi ya wawili ilipingwa sana, lakini faida yake itaonekana siku Mo akijikuta hana nguvu tena ya kuendeleza ufadhili wake. Kwa sasa Simba wanafurahia mafanikio ya muda mfupi kulingana na upepo wa kisiasa uliopo, ndio maana mpaka mashabiki wake wanatamba kuwa Simba ni serikali. Sasa kumbukeni yaliyopo yamekwisha kuwapo.

Kwa upande wa Yanga, mfumo uliopendekezwa na Rostam nadhani ndio sahihi kwa nature ya vilabu hivi. Tukubali tukatae, Mikia na Wananchi ni timu zenye mtazamo wa kisiasa zaidi kuliko michezo. Mkono wa siasa una nguvu mno kuliko uhalisia wa michezo, kiasi kwamba wanasiasa wamejinasibu wazi kuwa hawawezi kuziacha timu hizo. Sasa mwenendo huu ni adui mkubwa wa mafanikio ya muda mrefu kwenye michezo. Timu ya Yanga ijikite kuhamasisha wanachama, waanzishe kanzi data kama timu, wapate mapato kutokana na wanachama hao. Mfuno huu utafaa sana kwa muda mrefu, kama timu itaacha kusaka mafanikio ya muda mfupi ili kushindana na Simba.

Habari ya kuteka soko kwa soka la bongo ni upepo tu, siasa ndizo zitaamua.
 
Ukweli mchungu.
 
Reactions: Tui
Shadeeya njoo huku.Mwenzako anamuita Ali Mayai Tembele mamluki!!!Mtani wewe unasemaje?Au kisu kimegota mfupa. Sio kawaida yako mtani.
 
Umeandika mengi lakini fikra na msingi wa mawazo yako ni uleule unaokosolewa na mleta maada yaani fikra mgando za kizamani zisizozingatia Hali halisi na mahitaji ya Sasa.
 
Umeandika mengi lakini fikra na msingi wa mawazo yako ni uleule unaokosolewa na mleta maada yaani fikra mgando za kizamani zisizozingatia Hali halisi na mahitaji ya Sasa.
Umekariri kwa hicho ukisemacho. Jifunze mifumo ya soka ndipo useme fikra za kizamani, usikubali kusombwa na upepo tu. Tatizo la kwanza kwa soka la Tanzania ni siasa. Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…