Yanga itafute mwanasheria mwingine, iachane na Patrick Simon, ana kasoro

Yanga itafute mwanasheria mwingine, iachane na Patrick Simon, ana kasoro

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nimemsikia GB64 akitangaza mitandaoni kuwa wachezaji Yanga wanatumia dawa za kuongeza nguvu, ina maana Patrick Simon hazioni clips hizi?

Kama sio kweli anachosema GB64 kuhusu Yanga kwanini hafunguliwi mashtaka mahakamani kwa kuharibu brand ya Yanga?

Akina Magoma walifungua na kuendesha kesi inayohusiana na Yanga hadi wakapewa ushindi lakini Patrick Simon hakunusa kitu chochote kutoka Mahakamani wala kutoka kwa wanasheria wenzake kuwa kuna kesi inayoihusu Yanga.

Kesi ya Morrison kwenda Yanga, mkataba wa Fei Toto kwenda Azam, nk. Inaonekana Partick Simon hana uzoefu au hana weledi unaohitajika kwenye timu kubwa kama Yanga. Tatizo ni uongozi au ni Simon?

Ni heri aachwe akatafute changamoto nyinge kwingine na kutafuta mshauri mwingine wa kisheria wa timu.
 
What if anashauri na kuambiwa potezea maisha yaendelee. Yanga ka speed kale TU yahusishwe madawa hivi watu huwa hawaoni zile speed za epl UEFA champions league final ya man city na inter mpira ulikuwa Kasi hadi dk 45 hujui zimefikaje ndio ushangae speed ambayo tuliiona sababu Azam team ilikuwa hovyo kabisa mchezaji mwenye energy alikuwa Fei na Kipa na Fuentes angalia mechi na Apr Azam Wanacheza kama team ya umisseta
 
What if anashauri na kuambiwa potezea maisha yaendelee
Yanga ka speed kale TU yahusishwe madawa hivi watu huwa hawaoni zile speed za epl UEFA champions league final ya man city na inter mpira ulikuwa Kasi hadi dk 45 hujui zimefikaje ndio ushangae speed ambayo tuliiona sababu Azam team ilikuwa hovyo kabisa mchezaji mwenye energy alikuwa Fei na Kipa na Fuentes angalia mechi na Apr Azam Wanacheza kama team ya umisseta
kama unashauri kisheria na ushauri wako wa kitaaluma hautekelezwi kwanini usijiuzulu mwenyewe? kazi yako itakuwa nini?
 
Nimemsikia GB64 akitangaza mitandaoni kuwa wachezaji Yanga wanatumia dawa za kuongeza nguvu, ina maana Patrick Simon hazioni clips hizi?, kama sio kweli anachosema GB64 kuhusu Yanga kwanini hafunguliwi mashtaka mahakamani kwa kuharibu brand ya Yanga?. Akina Magoma walifungua na kuendesha kesi inayohusiana na Yanga hadi wakapewa ushindi lakini Patrick Simon hakunusa kitu chochote kutoka Mahakamani wala kutoka kwa wanasheria wenzake kuwa kuna kesi inayoihusu Yanga. Kesi ya Morrison kwenda Yanga, mkataba wa Fei Toto kwenda Azam, nk. Inaonekana Partick Simon hana uzoefu au hana weledi unaohitajika kwenye timu kubwa kama Yanga. Tatizo ni uongozi au ni Simon?

Ni heri aachwe akatafute changamoto nyinge kwingine na kufauta mshauri mwingine wa kisheria wa timu.
Sio lazima mwanasheria wa Yanga ndio afungue kesi, ata mwanachama hai yoyote kutokea tawi lolote Nchini anaweza Fanya hivyo.

Kwasasa ni kujisumbua kuwafungulia kesi wasema hovyo kwakua Mafanikiao ya Yanga Uwanjani Yana waumiza Wengi ki saikolojia.

Hali itakua mbaya zaidi uko tunapo elekea kwakua Yanga ime jiimarisha zaidi kwaiyo tunategemea Yanga kufanya vizuri zaidi na ilo lita zidisha msongo wa mawazo kwa wapinzani na maneno mengi ya hovyo.

Simba nao wakati Yanga wanatembeza bakuli walitamba Sana, ila tangu Yanga ilipo imarike ki uchumi siioni Simba iki mkaribia Yanga na Hali itazidi kuwa mbaya kwa Wana Simba na malalamiko lukuki.
Kumbukeni waloshindwa uwa na maneno mengi.
 
Internet imetoa uhuru kwa watu wote hata tahira nae anahaki ya kutoa maoni yake cha msingi awe na bundle........ Sasa GB64 ana level gani ya elimu...... yaani mtu aliyekaa darasani abishane na GB64 ni kuikosea heshima degree yake ya sheria. Then aje kubishana na magoma,anayetaka katiba ipigiwe kura na wanachama wote, wewe kwa akili yako umeona wapi ktk ya CCM au CHADEMA au taasisi yoyote katiba imepigiwa kura na wanachama wote? Bali ni wajumbe wachache wanao wakilisha matawi ndio watakaopiga kura kuwakilisha wenzao.Anaye msupport ni chizi kwani mfumo walio utumia Yanga ndio mfumo unaotumika taasisi zote.

Kwani Yanga ndio wa kwanza kushindwa kwenye mashauri.....?, vp shauri la Aweso, vip Lawi haya mashauri nayo hujayaona..... halafu nani aliye kwambia shauri la Fei Yanga walishindwa..... au umesahau Yanga walipewa ushindi mara tatu na TFF,ila kilicho kuja kuharibu tukaachana na uweledi na kuingiza siasa,sema tu FIFA hawakulijua hili,mdaa huu mngekula ban na kuishia kushiriki michuano yenu ya ndani.

Mnawasikiliza hawa wajinga wajinga sijui Chagamba,Kisugu,GB64 ambao hukimbilia kamera ila wanacho ongea nonsense, upuuzi upuuzi tu.
Mbona GB64 alikamatwa na kutiwa ndani na wanasimba wenzake kwa kuangalia clips zake tu? Mwanasheria wa Yanga inakuaje anakaa kimya wakati GB64 anaichafua taswira ya taasisi?

Mwanasheria wa taasisi ndiye mtu wa kwanza kulinda haki, mali na taswira ya taasisi, lazima atoe onyo au kushitaki watu wote wanaoisema na kuihujumu taasisi. Angemuomba GB64 athibitishe madai yake kuwa Yanga wanatumia dawa.
 
Sure GB 64 naona anatumia uchuchunge wake kuongea tu kwakuwa anashajenga jina ,mimi naona huwa ni mropokaji tu anaenda na jinsi wanasimba wanavyotaka naye anapita nao so wakimshangilia na yeye anapata bichwa.
Kama ni mropokaji tu basi asingekamatwa na polisi na kuwekwa ndani kwa maelekezo ya wanasimba wenzake. Simon hafai tu.
 
Nimemsikia GB64 akitangaza mitandaoni kuwa wachezaji Yanga wanatumia dawa za kuongeza nguvu, ina maana Patrick Simon hazioni clips hizi?, kama sio kweli anachosema GB64 kuhusu Yanga kwanini hafunguliwi mashtaka mahakamani kwa kuharibu brand ya Yanga?. Akina Magoma walifungua na kuendesha kesi inayohusiana na Yanga hadi wakapewa ushindi lakini Patrick Simon hakunusa kitu chochote kutoka Mahakamani wala kutoka kwa wanasheria wenzake kuwa kuna kesi inayoihusu Yanga. Kesi ya Morrison kwenda Yanga, mkataba wa Fei Toto kwenda Azam, nk. Inaonekana Partick Simon hana uzoefu au hana weledi unaohitajika kwenye timu kubwa kama Yanga. Tatizo ni uongozi au ni Simon?

Ni heri aachwe akatafute changamoto nyinge kwingine na kufauta mshauri mwingine wa kisheria wa timu.
Hv ina programm ya kupima wachezaji matumizi ya dawa zisizorusiwa michezoni (Enhacement drugs) hata mara 2 kwa msimu ?m
 
Sio lazima mwanasheria wa Yanga ndio afungue kesi, ata mwanachama hai yoyote kutokea tawi lolote Nchini anaweza Fanya hivyo.

Kwasasa ni kujisumbua kuwafungulia kesi wasema hovyo kwakua Mafanikiao ya Yanga Uwanjani Yana waumiza Wengi ki saikolojia.

Hali itakua mbaya zaidi uko tunapo elekea kwakua Yanga ime jiimarisha zaidi kwaiyo tunategemea Yanga kufanya vizuri zaidi na ilo lita zidisha msongo wa mawazo kwa wapinzani na maneno mengi ya hovyo.

Simba nao wakati Yanga wanatembeza bakuli walitamba Sana, ila tangu Yanga ilipo imarike ki uchumi siioni Simba iki mkaribia Yanga na Hali itazidi kuwa mbaya kwa Wana Simba na malalamiko lukuki.
Kumbukeni waloshindwa uwa na maneno mengi.
Mwanasheria wa club ni muhimu sana kipindi hiki kuliko huko nyuma tulikotoka. Kuna watu wamewekeza pasa zao nyingi sana kwaajili ya brands za timu. Hawezi kutokea mtu akaropoka tu bila kutoa ushahidi kuwa wachezaji Yanga wanatumia dawa au Simba wanapuliza dawa vyumba vya wapinzani viwanjani halafu mtu huyo akaachwa hivihivi.
 
Mzee wa KURJUANI anawapelekesha kisheria nasubiri EVICTION ORDER nione kama itakuwaje
 
Yale mashuti ya aziz ki lazima anatumia madawa ya kuongeza nguvu
 
Mbona GB64 alikamatwa na kutiwa ndani na wanasimba wenzake kwa kuangalia clips zake tu? Mwanasheria wa Yanga inakuaje anakaa kimya wakati GB64 anaichafua taswira ya taasisi?

Mwanasheria wa taasisi ndiye mtu wa kwanza kulinda haki, mali na taswira ya taasisi, lazima atoe onyo au kushitaki watu wote wanaoisema na kuihujumu taasisi. Angemuomba GB64 athibitishe madai yake kuwa Yanga wanatumia dawa.
Wanini kushindana na hasiye jihelewa,kwani mashabiki wangapi wanayo itukana 5imba kwenye hizo media,mbona mpaka sasa wapo. Halafu husifananishe Yanga na hao wengine kila chombo kina utaratibu wake.
 
Amekamatwa kwa kutenda jinai mkuu ,kama asingetenda asingekamatwa.
Kutumia dawa zisizotakiwa sio jinai? anajua ameumiza watu wangapi kisaikologia na kiuchumi na kijamii kwa kusema Yanga wanatumia madawa yasiyoruhusiwa michezoni? Mwnasheria wa Yanga kukaa kimya ni kukubaliana na madai ya GB64 kwenye hilo.
 
Wanini kushindana na ahasiye jihelewa,kwani mashabiki wangapi wanayo itukana 5imba kwenye hizo media,mbona mpaka sasa wapo. Halafu husifananishe Yanga na hao wengine kila chombo kina utaratibu wake.
Yanga sio mali ya mtu binafsi kuwa akiamua yeye kuvumilia basi inatosha. Yanga ni taasisi kubwa sana yenye wadau wengi sana wenye hadhi tofauti. Kiongozi wa yanga lazima awe na dhamana ya kulinda taasisi hii na mali zake na hadhi yake. Ukishindwa hilo ondoka mara moja kwenye taasisi hiyo. ndio maana wafadhili wote wakubwa wanawekeza Simba na yanga hata kama wana fedha za kuanzisha timu zao. KUItukana clubu hadharani na viongozi wakakaa kimya ni upuuzi.
 
Hivi kuna matahira wangapi kila baada ya mechi wanakimbilia kwenye kamera na kuitukana timu,maana kama ikiwa hivyo huyo mwanasheria atakuwa anashinda kwa pilato kila siku? Haya tokea aonge kuna impact gani iliyo ipata Yanga labda kiuchumi au uwanjani na nje ya uwanja?
 
Unataka mwanasheria wa taasisi kubwa kama yanga aanze kuwajibu hawo wehu wa Simba ambao hawajui hata msimu huu timu itamaliza nafasi ya ngapi?
Tunataka kiongozi wa timu awe proactive badala ya reactive, awe kama mbwa wa kunusa hatari ambayo haijatokea.
 
Back
Top Bottom