Hiyo sio kweli, ana akili zake, na akikosea anahukumiwa vilevile. Utani usivuke mipaka ya kisheria na kibiashara.
Mfano, Ally Kamwe kudanganya umma kwamba Yanga wamepokea taarifa rasmi kutoka CAF kuwa mechi yao dhidi ya Vital'O ndio iwe mechi ya ufunguzi rasmi wa mashindano ya CAF ni makosa kama atakuwa aliudanganya umma kwenye jambo hilo. Anatakiwa atoe ushahidi kama kweli CAF wameleta taarifa Yanga, vinginevyo atakuwa amesema uongo na mkutumia taasisi na madaraka kuudanga umma akiwemo Rais wa Jamhuri na wadui mbalimbali' amesababisha usumbufu kwa watu mbalimbali. Adhabu yake ndogo kuliko zote ni kupewa onyo kali na mamlaka zinazolinda afya na ustawi wa umma. Ni kauli ambayo imesababisha tahaluki.
Taasisi hizi za Simba na Yanga zisipewe watoto wadogo kuziongoza, zina wadau wengi sana wa levels tofauti, ukiwa kiongozi huwezi kujisemea chochote na lolote; unawezakusababisha maafa makubwa sana ndani ya jamii.