Yanga jikiteni zaidi kwenye mabadiliko ya timu sio ubingwa.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Msipokuwa makini kuna kila dalili ya kukosa vyote, ubingwa na mabadiliko ya mfumo wa club.

Nionavyo mimi tumieni nguvu zenu nyingi kufanikisha mageuzi ya mfumo wa uendeshaji wa klubu yenu badala ya kufarakana wakati wa kuutafuta ubingwa wa msimu huu unaokaribia kuwaponyoka.

Waambie mashabiki wenu ukweli kuhusu jambo hili kuwa Simba mfumo mpya wa uendeshaji wa club unawabeba hivyo watulie ili mfanikishe mageuzi hayo kwa pamoja.
 
Mkuu mbona nyuzi zako siku hizi unaandika kama vile unaikana Yanga, wote humu tunajua wewe ni shabiki wa Yanga, kwanini utumie misemo kama timu Yao na sio yetu, hebu ishauri timu yako ukiwa huru haina haja ya kujificha ficha baada ya mambo kuwa tofauti na matarajio yenu
 
Hata simba siimetoka sare na prison? Viongozi na mashabiki wa yanga Wamepanic tu kusema na kuyafanya yale baada ya sare
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…