Yanga kama Mwadui hucheza kumkamia Simba

Yanga haikukamia game. Hata saikolojia ya wachezaji uwanjani tu wakati Mpira unachezwa unaweza kujua Nani alikamia game.

Yanga wali relax Sana walicheza Mpira taratibu lkn kwa umakini mkubwa Sana.. Simba ilicheza Mpira wa nguvu bila kutumia akili ndio maana walitengeneza nafasi nyingi lkn upapara wa kumalizia ukikosekana ndio maana hawakupata matokeo

Halafu ipo hivi mathematically
Simba Ni timu mbovu Sana inapokutana na Yanga ligi kuu na Yanga Ni timu nzuri inapokutana na Simba. Lkn Simba Ni wazuri wanapokutana na timu zingine and virce versa Yanga Ni wabovu Sana wanapokutana na timu zingine tofauti na Simba. Kwahyo Simba wajipanga kidogo wapunguze presha wanapocheza na Yanga

Ushindi wa Yanga Jana unadhihirisha Ni kwa namna Gani ligi yetu ilivyokuwa Bora na Ni ya kiushindani kuliko Simba wangeshinda game ya Jana kutokana na Aina ya wachezaji wazuri ambao Simba wanao ambao hawaijui Derby ya Kariakoo. Ndo. Mana kimataifa Simba inaweza Fanya vizuri
 
Hivi, mnaposema kuwa Simba imepata mafanikio makubwa katika mashindano ya kimataifa waga mnamaanisha kufikia nusu fainali ya klabu bingwa Afrika mwaka 1974 na kutolewa na Mehalla El Khubra ya Egypt au kutolewa kwenye fainali ya kombe la Caf mwaka 1993 na Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Hatujawahi kuona kombe lolote la Afrika lililoletwa na Simba katika nchi hii. Lakini msichokijua ni kwamba Simba hii hii unayoiona leo imenusurika kushuka daraja mara mbili mwishoni mwa miaka ya themanini na kati ya hizo kuna moja waliokolewa na Yanga ila hayo hamuwezi kufahamu kwa sababu hayatawapendezea.
 
Naona mmevurugwa haswaaa. Poleni na nyie tuwapongeze kwa kujiamini kupita kiasi mkiongozwa na lopolopo wenu.
 
Mikia unateseka ukiwa upande gani wa nchi yetu pendwa?
 
Bila ushabiki hakuna cha upepo wala nini Simba ni bora kwa hapa Tz na Afrika mashariki.Kuwa na wachezaji wazee , uongozi mbovu , viwanja vibovu, hakuna fedha sio sababu ya kusema klabu fulani sio bora.Ubora wa klabu unapatikana kutokana na matokeo ya uwanjani . Ni simba tu ndani ya misimu mitatu kutoka Afrika mashariki ndio ilifuzu makundi CAF champions na kufuzu quarter final mara mbili, sasa unasemaje ni upepo? Huo upepo haupo Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda au pale jangwani?
 
Sijui kwa nini mawazo ya ovyo kuhusu mpira, mengi hutoka kwa mashabiki wa Simba.
 
Sahihi hasa kwa sisi tuliocheza mpira , tunajua maana hasa ya kukamia
 
Je, Simba ingeshinda ungesemaje?
 
Hongereni Yanga na poleni sana Simba. Timu zote zilipania kushinda lakini Yanga ilishinda kwa sababu walikuwa na mbinu nzuri uwanjani kuliko Simba. Na kama Yanga wangekuwa watulivu ubao ungesoma 3 - 0 ndani ya dakika 15 za mwanzo na mechi ingeishia pale pale. Benchi la ufundi la Simba lilikuwa limepigwa ganzi na halikujuwa lifanye nini ndani ya hizo dakika 15 wakati Yanga akiwa ana shambulia kwa kasi na kupata kona zaidi ya tano na kukosa magoli mawili ya wazi. Yanga waliizidi Simba kwa sababu walikuwa "direct" zaidi - pasi mbili ya tatu kwa Kisinda wameshafika golini lakini Simba wao kila anayepewa lazima aupake rangi kwanza halafu wakimpa Morison yeye anataka awapige chenga wachezaji wawili/ watatu wa Yanga kama anavyowafanya Gwambina anasahau ile ni "derby". Hata benchi la ufundi lilipoamua kuingiza washambuliaji watatu bado Simba walikuwa usingizini wanapiga pasi zao fupi fupi kwenye nusu ya kwao wakati washambuliaji wanasubiri mipira mbele.

Mechi ijayo Simba wajipange la sivyo watakufa tena Kigoma. Kitakachowaokoa ni kumuanzisha Morison benchi aingie baadae kwa sababu hakabi na pili anakaa na mpira muda mrefu bila sababu za msingi. Pia Morison ni mzuri akitokea benchi kwani timu pinzani inakuwa imeshachoka na anajua kusoma mchezo akiwa nje kabla ya kuingia na hili hata benchi la ufundi linajua. Pia viungo wao wakabaji wapeleke mipira mbele kwa haraka waachane na pasi fupi fupi kwenye "zone"yao. Ubaya wa pasi fupi ni kuwa bahati mbaya adui akiunasa mpira ni dhahama kwako na pia wakati unapiga pasi fupi fupi wachezaji wa timu pinzani wanakuwa wamesharudi golini kwao na kujipanga jinsi ya kuzuia. Na mtu wa kuwasaidia kwenye hili ambaye anaweza kupiga pasi za zaidi ya mita 30 kwa usahihi ni Saidi Hamis Ndemla ambaye benchi la ufundi limeamua kummaliza benchini sidhani hata kama akipangwa Kigoma atakuwa sawa labda wanze kumtumia kwenye hizi mechi chache za ligi kabla ya kwenda Kigoma.

Kwa aina ya mpira ambayo Simba walicheza juzi hata wakirudiana na Yanga mara kumi watapigwa tu labda wabadillike. Simba mara nyingi wanapata shida wanapokutana na timu zinazotumia nguvu na zile timu zenye kasi na bechi la ufundi halina kabisa "plan B" linapokutana na mpinzani wa aina hii.
 
Mbumbumbu Fc wanaumiaaaa, na Kigoma tunayapiga tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…