Yanga katika vita kubwa Kombe la Shirikisho leo

Yanga katika vita kubwa Kombe la Shirikisho leo

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
338
Reaction score
180
WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Yanga, leo wako ugenini jijini Accra, Ghana kwa kazi moja tu – kupata ushindi dhidi ya Medeama ya huko ili kujinasua kutoka mkiani.

Vipigo viwili mfululizo vya bao 1-0 kutoka kwa MO Bejaia ugenini na TP Mazembe nyumbani vimeipa kazi kubwa Yanga kuweza kuonyesha makali yake huku sare ya nyumbani dhidi ya Medeama nayo ikipunguza uwezekano wa timu hiyo kutoka jijini Dar es Salaam kufanya vyema zaidi.

Soma=> Yanga katika vita kubwa Kombe la Shirikisho leo | Fikra Pevu
 
Mechi ya Yanga vs Medeama inarushwa ss9 ila kwa anaejua fta channels itakayokua live atujuze
 
Mechi ni saa 9 mchana saa za kwao sawa na saa 12 jion saa za bongo
 
upload_2016-7-26_0-54-34.png

Hatuna budi kuiombea Yanga leo, Mwanahabari huyu kaitendea haki jamii ya wanamichezo Tanzania kwa kuripoti kitu halisia kilichopo.
 
Mechi itaonyeshwa chaneli gan?

Super Sports 9 ( japo Azam wataibia kama kawaida yao ) na muda ni Saa 12 kamili huku kwetu Tanzania ambapo kule kwao ni Saa 9 alasiri. Una swali jingine sijui Mkuu?
 
labda ZBC2 wataonyesha, stationi hii ipo kwenye vingamuzi vya Azam Tv na Contnental Decorder.

Imekuwa ikionyesha mechi hasa ya tim zetu zinapocheza iwe ugenini au nyumbani.

Tbc ni kama haipo imeshatupa kando mambo ya michezo.
 
WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Yanga, leo wako ugenini jijini Accra, Ghana kwa kazi moja tu – kupata ushindi dhidi ya Medeama ya huko ili kujinasua kutoka mkiani.

Vipigo viwili mfululizo vya bao 1-0 kutoka kwa MO Bejaia ugenini na TP Mazembe nyumbani vimeipa kazi kubwa Yanga kuweza kuonyesha makali yake huku sare ya nyumbani dhidi ya Medeama nayo ikipunguza uwezekano wa timu hiyo kutoka jijini Dar es Salaam kufanya vyema zaidi.

Soma=> Yanga katika vita kubwa Kombe la Shirikisho leo | Fikra Pevu

Nawatakia kila la kheri Yanga huko Takorada city leo na kama wakifanya haya yafuatayo nina uhakika Yanga itafanikiwa:
  1. Wacheze team work muda wote wa mchezo.
  2. Wachezeshe wingers wenye speed kama Mahadhi na Msuva ili wawachoshe half backs wa Medeama na wasiweze kupanda.
  3. Obren Chirwa na Donald Ngoma wawe twin strikers leo na Amisi Tambwe " akodoe " kwanza benchini.
  4. Iwe isiwe lazima leo mwenye timu yake Haruna Fadhil Hazikimana Niyonzima aanze na mbele yake awepo " fundi " mwenzie Thabani Kamusoko kwani mechi ya Dar Kiungo cha Yanga kilikufa " kibudu ".
  5. Oscar Joshua asianze na ikibidi hata Jezi asivae leo na nafasi yake acheze Mbuyu Twite hasa kwa sifa yake kuu ya kuwa all rounder player na ninaamini ataimudu vilivyo.
  6. Japo kwa sasa Yanga hawamuamini Nahodha wao Nadir Haroub Cannavaro ila kwa aina ya " shughuli " yake ya KAZI KAZI na ule uhamasishaji wake leo ana umuhimu mno aanze na acheze dakika 90 kama hatopata maumivu yoyote.
  7. Mabeki wa kati, kushoto na kulia wasisahau muda mwingine kuwachezea hawa Madeama mpira wa Ndondo ili kuwatisha kama ambavyo Kelvin Patrick Yondani alivyokuwa akiwafanyia hapa Dar kwa kuwapiga piga " brush " kila mara Wachezaji wa Medeama hadi wakawa kila wakienda golini kwa Yanga wanamuamkia Shikamoo Kelvin Yondan kisha wanamuachia mpira kwa kumuogopa. Beki unatakiwa " utishe " siyo unacheza tu " kinyoro nyoro ".
Japo nikiri kabisa na najua wengi mnanijua kuwa Mimi ni Simba Sports Club wa KINDAKI NDAKI kabisa ila kama leo Wachezaji wa Yanga watakaza ile kisawa sawa sina wasiwasi kuwa leo Yanga itatushangaza wengi kwa kuibuka na ushindi.

Kila la kheri Yanga Football Club.
 
Back
Top Bottom