Yanga kubandua nembo ya Haier kimkataba

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

Wakati mtaani watu wanasema kwenye mashindano ya kimataifa Sportpesa hawatoi hela.

Kwenye mkataba wa Yanga SC na SportPesa katika hatua hizi za makundi, robo fainali, nusu fainali na fainali kuna bonasi kutoka Sportpesa kwenda Yanga SC iwapo watashinda mechi, kuingia robo fainali, kuingia nusu fainali, kuingia fainali na kuchukua ubingwa.

Sasa kama mdhamini analipia yote hayo na anakuambia hataki uweke kitu kingine hapo unawezaje kumkiuka?

Wakati mwingine tufanye mambo kisasa kidogo, nafahamu Yanga SC na SportPesa walikuwa kwenye majadiliano Yanga wakiomba kutumia eneo ambalo SportPesa wanastahiki kuwepo kimkataba.

SportPesa wakakataa kwamba hawapaswi kufanya hivyo.

Kimkataba pia SportPesa wanahaki ya kusema nani awekwe hapo nani asiwekwe na kila upande unafahamu hilo.

Unabaki unajiuliza haya yametokeaje ili hali mkataba ni makubaliano ya kisheria ambayo yanapaswa kuheshimiwa na pande zote zilizomo kwenye huo mkataba?

Kuna mahala pana tatizo ingawa hatutaki kukubali na kusema ukweli.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)
 
Yanga wamezingua kwenye hili. Aliyepaswa kuingia Makubaliano na hao wadhamini wapya ni Sportpesa, siyo Yanga. Au Yanga walitakiwa kuwashawishi Sportpesa bila kuchoka hadi Wakubali.

Walichokufanya Yanga ni sawa ni zile guest za vichochoroni. Unalipia chumba ukitoka kwenda kwenye mishe zako wanakitumia kwa kuwauzia wale wa shorttime (Chapchap)

Uongozi wa Yanga unatakiwa ujifunze kutofautisha kati ya biashara na ushikaji walio nao na Mkurugenzi wa Sportpesa na Uanachama wake kwa Yanga.

Mwisho Mashabiki na Wanachama wa Yanga na Simba wajifunze kuongelea na kukosoa vikali na kutoa ushauri pale uongozi unapokua unafanya mambo ya Kihuni yasiyo na afya kwa soka, badala ya kuacha kazi hiyo ifanywe na wapinzani wao huku wenyewe wakiwa busy kutetea ujinga.

Katika hili niwapongeze Kwa dhaati sana GENTAMYCINE na MTAZAMO
 
juzi tu wame toka kulia lia fei haja fuata mashart ya mkataba sasa wao na upuuzi uleule kwa mdhamin wao
 
Wengi wanashindwa kulitambua hili wamekomaa na bonus kama ndio big issue wakati ni reward isiyokuwa ya lazima
 
Yanga na mikataba kila siku drama

CAS yanga vs morrisson sababu mkataba

Yanga vs Fei toto sababu mkataba

Yanga vs sport pesa sababu mkataba

Kama yanga watashindwa na sportpesa natoa Ushauri kwa yanga ibadili legal department yake inapwaya sana
 
Nilitegemea nitakuta vipengele vya mkataba umewekwa hapa kubainisha hizo bonus za mashindano ya kimataifa. Kumbe maneno matupu
 
Ndoige

Akibandua anapata hasara, Akiacha anapata hasara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…