View attachment 2503200
Wakati mtaani watu wanasema kwenye mashindano ya kimataifa Sportpesa hawatoi hela.
Kwenye mkataba wa Yanga SC na SportPesa katika hatua hizi za makundi, robo fainali, nusu fainali na fainali kuna bonasi kutoka Sportpesa kwenda Yanga SC iwapo watashinda mechi, kuingia robo fainali, kuingia nusu fainali, kuingia fainali na kuchukua ubingwa.
Sasa kama mdhamini analipia yote hayo na anakuambia hataki uweke kitu kingine hapo unawezaje kumkiuka?
Wakati mwingine tufanye mambo kisasa kidogo, nafahamu Yanga SC na SportPesa walikuwa kwenye majadiliano Yanga wakiomba kutumia eneo ambalo SportPesa wanastahiki kuwepo kimkataba.
SportPesa wakakataa kwamba hawapaswi kufanya hivyo.
Kimkataba pia SportPesa wanahaki ya kusema nani awekwe hapo nani asiwekwe na kila upande unafahamu hilo.
Unabaki unajiuliza haya yametokeaje ili hali mkataba ni makubaliano ya kisheria ambayo yanapaswa kuheshimiwa na pande zote zilizomo kwenye huo mkataba?
Kuna mahala pana tatizo ingawa hatutaki kukubali na kusema ukweli.
BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)