Yanga kuchagua manahodha bila kuwa na Kocha Mkuu ni kukurupuka

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kuna wakati unashindwa kuelewa kile wanachokifanya uongozi wa Yanga. Iko siku uongozi huu utaingia kwenye ugomvi mkubwa na wanachama na wadau wa Yanga.

Matukio ya hovyo mpaka sasa chini ya uongozi huu:

1. Kumpoteza Beno Kakolanya
2. Kufujuza mpambanaji Zehera
3. Kuwafukuza akina Balinya
4. Ugomvi na Molinga aliyekuwa anainusuru timu
5. Kufanya usajiri wa wachezaji bila ya matakwa na uwepo wa kocha Mkuu
6. Kumpoteza Morrison
7. Msimu kuanza bila ya jezi ya msimu
8. Kumfukuza Eymael katikati ya usajili
8. Kumfukuza Zlatic baada ya mechi aliyoshinda 3-0 na karibu ya mechi kubwa ya Simba na Yanga.
9. Sasa kuchagua manahodha bila uwepo wa kocha Mkuu kwenye club.

Kuchagua manahodha muda mfupi kabla ya kocha Mkuu kuwasili ni kumtafutia ubaya kocha anaekuja. Kwani nahodha ni lazima awe mtu anayependwa na kuaminiwa na kocha kutokana sababu na vigezo vya kocha mwenyewe.

Sina ugomvi na Lamine, lakini Lamine ni mchezaji ambaye alishawqhi kuikimbia Yanga hivi karibuni, sio mvumilivu, iko siku anaweza kuwashawishi wenzake watimke Kama malipo yatachelewa.

Kulikuwa na haraka gani kumsubiri kocha Mkuu aje ashiriki kumchagua nahodha? Utakuwa ugomvi miongoni mwa wachezaji kama kocha mpya atakuja kutengua maamuzi ya viongozi na kuchaguwa wa kwake.

Siku nyingine tusichague kiongozi wa club ambaye ni kocha pia.
 
Yule jamaa aliyewaita UTOPOLO apewe PhD yake plz cc Shadeeya
 
Mwenyekiti ana taluuma ya ukocha, kwahiyo hujiona kocha bora kuliko kocha mwenyewe.
 
Mwenyekiti ni Kioja.
Anataka kufanya mambo matatu kwa wakati mmoja.
Kocha, Mkurugenzi wa ufundi na Mwenyekiti wa klabu.
Anawakera makocha. Hata Zahera aliwahi kulalamikia vitendo vya kuingiliwa kwenye mazoezi na upangaji wa kikosi. Hasara ya kumsajilia mwalimu wachezaji Ni mwalimu kutumia muda mwingi kutafuta combinations.
 
Mtani huoni kwamba italeta mgogoro na vinyongo?? Ndio maana nilisema Yule jamaa aliyewaita UTOPOLO apewe PhD yake!
Mgogoro kwa nani sa Mtani wakati Kocha ana maamuzi yake ambayo kwa kila mchezaji mwenye akili timamu atakuwa analijua hilo na ndio sababu waeza kuta mchezaji ana namba kwa kocha huyu ila akija kocha mungine anaishia kukalia benchi.
 
Mgogoro kwa nani sa Mtani wakati Kocha ana maamuzi yake ambayo kwa kila mchezaji mwenye akili timamu atakuwa analijua hilo na ndio sababu waeza kuta mchezaji ana namba kwa kocha huyu ila akija kocha mungine anaishia kukalia benchi.
Fikiria wewe umeteuliwa na Mkuu wa wilaya kuwa katibu kata lakini akaja Mh. Diwani akatengua uteuzi wako kwasababu zake na kumpa mfanyakazi mwingine hapohapo kwenye ofisi ya kata. Je, hutauliza sababu ya Diwani kutengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya? Je, aliyechukua nafasi yako hutamuona Kama chanzo Cha kutenguliwa kwako

Je, aliyeteuliwa atakuwa rafiki yako mkubwa?
 
Haya mnayawaza nyie ilimradi tu kionekane kilichofanyika si sahihi.

Ila mwisho wa siku niseme tu hamna jipya ambalo Yanga kafanya hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…