YANGA: Kuelekea mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji

Easyway

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
2,606
Reaction score
3,710
Klabu yetu inategemea kuanza mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu, kwa mujibu wa mwenyekiti Dr.Mshindo Msola mchakato unategemea kuanza may 2020.

Kimeandikwa kitabu kinachouzwa sh.5000, ili Wanachama wa Yanga wapate uelewa wa mambo yote yanayohusu uwekezaji na aina ya uwekezaji kwenye vilabu vya mpira wa miguu Duniani,maana ya hisa na aina za hisa, faida itakazopata klabu hiyo itakapokuwa imeingia kwenye uwekezaji,changamoto itakazokutana nazo klabu ya Yanga itakapoanza mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeahaji na namna ya kutatua changamoto hizo.

Wanachama,mashabiki na wapenzi wa klabu ya Yanga wanatakiwa waelewe kwa kina masuala hayo ili waweze kupokea mabadiliko kwa mikono miwili na pia ili wasiachwe nyuma kwenye mchakato mzima wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu yao.
Kitabu kinapatikana DSM mtaa wa Livingstone,kwenye kibanda Cha Mpesa kinachotizamana na duka la Dubai kitchen party.
Kwa mikoani kinatumwa ,0713925634.

Daima mbele nyuma mwiko.
Idumu Timu ya wananchi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka enzi za tarimba huu mchakato ulikuwapo. Hii kweli ndio yanga!
 
Kikosi cha Tar.8. Kikosi kilichomtoboa Aishi Manula ndio maana mashabiki wa Simba lazima waonekane km mashahidi.
Hapo kwenye picha naona wachezaji wa Yanga ila background kuna Simba.

Daima mbele nyuma kuna mwiko[emoji1787]

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye picha naona wachezaji wa Yanga ila background kuna Simba.

Daima mbele nyuma kuna mwiko[emoji1787]

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
Hiyo picha ilipigwa tarehe 8 march 2020 kwahyo ni muhimu background kuwa hivyo kama ukumbusho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Itakua ahueni ili wale simba wa maonesho wakose cha kututambishia. Wametunyanyapaa sana msimu uliopita. Na tusingewafunga kwenye mechi ya mwisho kukutana, ndiyo tungeishi maisha magumu kwelikweli.
 
Kati ya kitu ambacho wapenzi wa Simba hawataki kikisikia ni Yanga kubadili mfumo.
Maana wanajua zile zama za Yanga kuchukua kombe mfululizo zinarudi, Yanga ile ya kuchukua kombe mfululizo inarejea.
Yanga iliyokuwa inampiga Simba inavyotaka, Yanga ya kampa kampa tena,na naomba kombe la Azam tukutane na mikia tumpige tena kidude.
Wananchi tukae mkao wa kula, kuanzia msimu ujao ni kunenepa tu, dalili njema huonekana asubuhi tumuunge mkono Msola tumuunge mkono GSM, safari hii lazima kieleweke.
Kitu kizuri uwekezaji wetu hautakuwa wa ujanja ujanja kama wa Simba,wakiulizwa bilioni 20 zipo wapo hakuna anayejua zilipo,utasikia sisi tunataka furaha tu.
Tusome kitabu ili tujielimishe tusije tukawa kama mikia isiyojua chochote kuhusu uwekezaji wao.
Sina hofu wala shaka safari hi Yanga tutabadilisha mfumo na tutapata mwekezaji mzuri na msimu ujao Ya nga bingwa.
Daima mbele nyuma mwiko.
Idumu timu ya wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umbumbumbu wenu upo damuni siku hizi
Kwani watunzi wanaoandika vitabu vyao vya elimu mbalimbali na kuingiza sokoni wanafanya kwa kujifurahisha na sio biashara? Wakifanya bure hizo gharama za uchapishaji zitarudi vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie ndio mbumbu mpaka hapo hamjui jamaa anapiga pesa kwa kuwauzia vitabu
 
Hapo kwenye picha naona wachezaji wa Yanga ila background kuna Simba.

Daima mbele nyuma kuna mwiko[emoji1787]

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
Hiyo Picha ma mbumbumbu Kama wewe inawauma sana maana hiyo tarehe kamwe itabaki kwenye vichwa vyenu: Chetu Chetu.....in.... Voice
 
Ubarikiwe mkuu
 
Hata mimi nakitaka hicho kitabu ili nipate elimu ya uwekezaji ni nini pengine na mimi naweza nikaja kuwa na hisa ndani ya hizo 51 za wanachama.Nyie watu wa simba endeleni kupinga tu wakati hamjui hili wala lie juu ya uwekezaji na hamjui mchakato mzima una face ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…