Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Habari zenu wana michezo mliomo humu ndani, hakika msimu wa mwaka 2020/2021 umeisha na pongezi kwa timu zilizoweza kufikisha malengo kwa asilimia mia moja na waliokaribia asilimia mia. Ila pole kwa walioshindwa kutimiza malengo yao na niseme tu nafasi ya kujipanga kuelekea msimu mpya ni huu.
Twende moja kwa moja kwenye mada. Binafsi kama shabiki wa Yanga kuna vitu nilivitegemea kufanyika kabla la jambo lolote ile kama kweli uongozi wa Yanga upo serious juu ya kufanya vyema katika msimu mpya ikiwa pamoja na kuijenga timu kiushindani.
Baada ya mchakato wa mabadiliko kukamilika kisha washabiki, wanachama, serikali na wadau wengineo kuridhia na kubariki mchakato wa mabadiliko nilitegemea Yanga iingie katika mfumo rasmi kabisa kulingana na katiba yao mpya inavyosema ikiwa pamoja na kuwapa timu hao wawekezaji, na kuundwa kwa uongozi mpya kulingana na katiba mpya ya Yanga.
Sasa ni jambo la ajabu mchakato umekamilika lakini hakuna kinachoendelea, wanaoendesha usajili ni wale wale akina GSM wa siku zote inamaana Yanga inaanza msimu kwa strategic zile zile za misimu ya nyuma. Ila mfumo mpya ungekuwa umeanza pengine huyo Makambo asingechukuliwa wangekuja wachezaji ambao ni zaidi ya makambo kwavile tu tayari wawekezaji wameshaweka fungu kubwa kwaajili ya usajili hivyo wangesajili kwa matakwa ya ripoti ya benchi la ufundi. Huu ndio ulikuwa wakati sahihi kwa mfumo mpya kuanza sasa.
Kwa wale wanaotegemea makubwa kutoka kwa Yanga msimu wa 2021/2022;basi mjiandae tu kwa maumivu maana mambo yanaendelea katika yale yale ya misimu ya nyuma. Yanga imefanikiwa kusaini dili nono na Azam ilikuwa ni wakati sahihi sasa kuwa na wawekezaji na uongozi mahiri wanaoweza kupangilia contents nzuri na pia kuanza kuonesha update za miradi mbali mbali. Hiyo miradi yote inahitaji ela sasa kutoa ela kwaajili ya kufanikisha miradi hiyo ni moja ya majukumu ya wawekezaji.