Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,347
- 5,986
YANGA imepanga kufunga usajili wake mpaka kufikia mwisho wa wiki hii, lakini vifaa vitakavyohitimisha zoezi hilo la usajili vimewekwa wazi na kuonekana kwamba vitakuwa na ushindani mkubwa.
Katika usajili wa kiungo mkabaji mtihani mizito utakuwa ni kati ya kiungo raias wa DR Congo, Kabamba Tshishimbi anayechezea Mbambane Swallows ya Swaziland ambaye sasa nafasi yake inasubiri ubovu wa Mcameloon Fenando Bongnyang.
Bongnyang ambaye tayari yupo nchini akijaribiwa na kocha George Lwandamina, tayari alianza kumshawishi kocha huyu kutokana na utulivu wake na rekodi zake ambapo ataonyesha kumudu majukumu yake uwanjani anaweza kupewa usajili na kuzima ndoto za Kabamba kutua Yanga.
Tayari Lwandamina alishamuona Kabamba kwa awamu mbili tofauti ambapo anachofanya sasa ni kushindanisha ushindani wa wawili hao na kufunga usajili wa seheme hiyo ya kiungo kwa mchezaji wa kigeni akitakiwa kiungo wa shoka kwa kukaba na kupiga pasi za kuanzisha mashambulizi.
Mchezaji kiraka Erasto Nyoni wa Azam FC wakati wowote anaweza kumharibia Deus Kaseke kubaki kwenye timu hiyo baada ya mabosi wa Yanga kuchoka usumbufu wa kiungo huyo akiitaji fedha nyingi ili asaini.
Mazungumzo ya Yanga na Kaseke yameingia kwenye utata mzito ambapo mabosi wa Yanga wameanza kupiga akili mpya wakimfuata Nyoni ambaye wamegundua ana faida nyingi akiwa kwenye kikosi kutokana na kucheza nafasi nyingi akimzidi Kaseke.
Endapo Yanga itamalizana na Nyoni, ni wazi kwamba Kaseke anaweza kujikuta ghafla kaondolewa katika kikosi hicho baada ya kufanya kosa la kugomea kiasi cha fedha ambacho Yanga ilitaka kumpa ambazo ni zaidi ya sh mil 30.
Kiungo wa Mbeya City, Rafael Daudi ni kama tayari ameshavaa jezi za timu hiyo baada ya Yanga kumaliza kumuingizia fedha zake sambamba na kumalizana na klabu yake ya Mbeya City ambayo ilishapewa chake katika kumuachia kinda huyo.
Tayari taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Yanga, Husen Nyika alikuwa jijini Mwanza wikiendi iliyopita akivamia kambi ya Taifa Stars kumalizana na Rafael na Nyoni ambao walikuwa katika kikosi hicho walipocheza dhidi ya Rwanda.