Wakati mwingine, muwe na aibu japo kidogo, na muwe na heshima. Kazi kusifia vyenu, hata vinukavyo harufu mbaya!
Wewe umekuwa bingwa mara 30. Mwenzio mara 22. Wewe umeshiriki ligi ya mabingwa mara nyingi, kuliko mwenzio, tena tukiwakilishwa na timu moja. Mwenzio kaingia makundi mara nyingi kuliko wewe!
Kwa idadi ya ubingwa wako wa hapa Tanzania, na idadi ya uwakilishi wako wa kwenye mashindano hayo, ulitakiwa kwa sasa, pointi zako uwe umekaribiana na Al Ahly huko!
Cha kuchekesha, unamcheka uliyemzidi umri, na amekuzidi mali, kuwa unakaribia kumzidi!
Hamnazo kweli!