Shida ya team zetu zote tu naongelewa kwa ujumla, wakisajili mchezaji wanampa ustar kabla hata hajaonesha kitu uwanjani nadhani na hii inachangia sana wachezaji kufail. Mpira wa sasa sio wa miaka ya 80 mpaka 90 maana tuliegemea Radio na magazeti tu, sasa mtangazaji akitaka kumkuza mtu sisi sote tunamuamini na kujengwa taswira ya mchezaji sio wa kawaida. wangapi tumewatukuza wachezaji zamani na sifa kibao na wengi mpaka wameacha mpira hatukuwahi kuwaona wakicheza. Anyway kwa ufupi kusajili sawa ila kama mchezaji hajathibitisha kama bora tumwache kwanza aoneshe uwanjani atatukuzwa tu bila promo maana mipira tunaiona hatutegemei Radio tu tunaona live, labda kama tumesajili mchezaji toka team kubwa na kishaonesha yeye ni nani hapo tufanye mbwembwe zote ila hawa kama betting tuache kwanza.