Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,555
- 4,118
Yanga ni timu bora sana, tumeshindwa kufuzu robo fainali Klabu bingwa Africa sababu ya kupoteza kizembe mchezo wa kwanza nyumbani dhidi ya Al Hilal na baadae kufungwa ugenini na Mc Alger hivyo kulazimika kucheza kwa presha kubwa na ufundi kupungua kwenye mechi zilizokuwa mbele yetu.
Tukumbuke kuwa mechi za mwanzo klabu bingwa tulifungwa kwa kuwakosa mabeki wetu imara zaidi Job na Baka ikimaanisha kuwa kocha mpya Saed Ramovich anapaswa kuwapumzisha hawa vitasa katika mechi ndogo na kuweka wale wasiocheza kama Nondo, Gift, Andambwile, Mkude, Sureboy , Farid, Shehani, Nkane na Kibabage ili na wao wawe fit mda wote ili wapambane inapotokea wanalazimika kuwepo mechi kubwa, hili ni kosa la Gamondi kuchezesha kikosi kimoja kila mechi na kukosesha fitness wachezaji wa benchi , kosa lisilopaswa kuendelezwa , Yanga ina kikosi kipana ni vizuri wachezaji wote watumike ili wawe fit mda wote kukabiliana na mechi yoyote inapobidi.
Hakuna mchawi, hakuna lawama, tayari tumetolewa tujipange upya, biashara ni asubuhi, tulichemka wenyewe, hatukufanya maandalizi sahihi yanayoendana na ukubwa wa mashindano ya klabu bingwa Africa, tumepoteza leo ila tumejifunza pakubwa sana kuwa morali ya wachezaji lazima iwe juu kuanzia mechi ya kwanza na lazima tushinde mechi mbili za mwanzo , Yanga tuna uhakika msimu ujao tumo tena Klabu bingwa Africa , ujinga wakati wa kwenda, basi tukapambane kuanzia mechi za mwanzo kufia uwanjani kama jinsi tulicheza na TP Mazembe kwa Mkapa kwa ari kubwa nami nilikuwemo uwanjani na wanangu wakipuliza mavuvuzela kwa nguvu, msimu ujao klabu bingwa Africa ni lazima tuvune points 6 mapema. Ni lazima tushinde mechi tatu jumla, Yanga ni timu kali, uwezo huo wa kushinda tunao wachezaji wakiamua kujitoa, Mechi zile mbili za mwanzo tulipaswa kuvuna angalau points 4! Tunaomba wachezaji waamue kufungwa tena nyumbani iwe mwiko. Ni vizuri wachezaji wakitambua kufungwa nyumbani haikubaliki na huondoa mzuka wa mashabiki kuja uwanjani. Ushindi pekee huleta mashabiki uwanjani, wachezaji wanao huo uwezo wa kushinda timu yoyote iwe kubwa au ndogo wakiamua , kama jinsi niliona walipocheza na mazembe, kila mchezaji aliitaka mechi, moto wa siku ile ndio Yanga ninayoijua hakuna kushindwa, timu kubwa Africa na duniani unafungwaje kizembe na Al Hilal, tena kwenu? Hii haikubaliki. Hii haipaswi kutokea tena.
Soma Pia: FT: Yanga 0-0 MC Alger | CAF Champions League | Estadio Benjamin Mkapa | 18.01.2025
Leo haijauma sana sababu hesabu za calculator na kikokotoo huwa hazina guarantee, ni pata potea. Na kweli tumeliwa kichwa ila sio mwisho wa safari.
Hongera sana wachezaji wa Yanga mmepambana sana ila mlitukosea sana mashabiki baada ya kuruhusu kizembe kufungwa mechi ya kwanza tena nyumbani na hapo binafsi nilijua msimu huu si wetu na niliongea humu jukwaani kuwa tuko fungu la kukosa, I am now at peace because tumevuna tulichopanda. Binafsi nilijua hatutoboi na nilisema humu jf na ndicho kimetokea.
Yanga tumepata kocha bora, Saed Ramovich ni mtu na nusu, makali yetu yataleta kilio kwa kila mpinzani , ni suala la muda tu, kombe la klabu bingwa Africa ni mali yetu.
Tukamalize hasira kwa kuvunja vunja makolo kwenye derby na kubeba kombe letu la NBC premier league.