Msitafute mchawi yote haya yamesababishwa na mambo yafuatayo;
1.Usajili wa kukomoana(mihemko).Hakukuwa na haja ya Yanga kuwasajili Chama , Baleke na Dube . Hizo sajili zililenga kuwakomoa simba na Azam lakini ukweli ni kwamba uwezo wao kwa sasa ni mdogo mno.
2.Unywaji wa supu ya vibudu kupita kiasi.Mungu hapendi hii kitu ila mnalazimisha tu. Wachezaji walilewa sifa na kujiona wanaweza Sana wakasahau majukumu yao
3.Ununuaji wa mechi kwa timu za ligi kuu ya NBC umewafanya mjione mna timu nzuri kumbe ushindi wa mchongo hali inayosababisha mshindwe kubaini madhaifu yenu.
4.Marefa wa NBCPL wamewadekeza Sana wachezaji wenu . Hata wakifanya makosa ya wazi wao ni kufunika tu.Rejea mechi ya simba vs Yanga , Kibu alifanyiwa makosa zaidi ya mara mbili ndani ya 18 lakini Kayoko akapeta.Hali hii husabisha washindwe kujiamini wanapochezeshwa na marefa wa nje.
5. Timu ina vibabu wengi mno. Chama 37+
Aucho 37+
Dube 33+
Boka Njolinjoli 32+
Pacome 32+
Diara 33+