Yanga kutupwa nje ya Azam Conf. Cup

Mwaka jana Lipuli alifanyiwa hujuma ,na mara nyingi wanabadilisha kanuni,ila kama wanafuata kanuni kweli Simba akichukua ubingwa wa pande zote anayeenda confederation ni mtu wa pili kwenye msimamo wa VPL na siyo aliyetolewa kwenye Azam Cup.

Kwahiyo bado ligi inaendelea kwa nafasi ya 2,3 na 4.
 
Nafasi ya 3 & 4 mwaka huu haziwezi kuwa deal! Mwaka jana zilikuwa deal kwa sababu tulikuwa na wawakilishi 4 kwa makombe ya Afrika; kwa bahati mbaya, wote waliishia nafasi mbaya na hivyo hatuwezi kupata ile favor ya mwaka jana ambayo ilichangiwa sana na Simba kufika Robo Fainali na vi-point vichache vya Yanga ambavyo alivipata kwenye kufikia 16 bora kama sikosei!!

Ingekuwa mtarajiwa wa #2 VPL ingekuwa timu chovu chovu kipesa tungesema mtu unaweza kuendelea kufukuzia #3 ili namba #2 akishindwa kushiriki kutokana na ukata, basi #3 anaenda!!

Luck enough, #2 ni ama Azam, Yanga au Namungo, na wote hao uwezo wanao!
 
Mkuu hawa jamaa ni kama wamechanganyikiwa ,,,,,wao wanachofikiria Ni tarehe 8 tuu nafikiri ndio walimaliza ligi
 
Ligi yoyote bingwa akishajulikana tu tayari inakosa msisimko hasa ukizingatia nafasi ya 2 na 3 hazina faida yoyote! Ingekuwa kama zamani kwamba 3 Bora wanaenda Ligi ya Muungano, bado kipute kingekuwa kikali!
kwani ile nafasi ya Libya ya kuwa na timu 2 tumepokonywa?
 
kwani ile nafasi ya Libya ya kuwa na timu 2 tumepokonywa?
Ile nafasi inatokea baada ya ku-perform vizuri msimu uliotangulia kwenye Club Bingwa na Shirikisho! Unfortunately, msimu huu Simba katolewa mwanzoni kabisa na Yanga mwenyewe ndo hivyo tu!

Club Bingwa ndo kunatoa points nyingi zaidi, sasa ile wakilishi 2 tuliyokuwa tumepata msimu huu ni kutokana na Simba kufika robo fainali, Yanga nae alichangia vi-point vichache ambavyo vilitokana na kuingia 16 Bora Shirikisho!
 
yote hayo nilisikia bado pointi zilitosha mwakani
 
Ni kwamba aliyetuzidi point ambaye katupokonya hiyo nafasi amekuwa disqualified kushiriki mashindano yoyote ya CAF. so swali ni kwamba tutapanda sisi tunayefuatia?
 
yote hayo nilisikia bado pointi zilitosha mwakani
Inawezekana lakini sio guaranteed. Inawezekana kwa sababu wanaangalia performance ya miaka 5 iliyopita na msimu ambao Simba ali-perform bado upo within the past 5 years.

Hata hivyo sio guaranteed kwa sababu inategemea na performance ya nchi zingine. Sasa kama wale waliokuwa chini yetu msimu uliopita wameendelea kufanya vibaya zaidi, ina maana sisi tutaendelea kubaki position ile ile. Lakini kama waliokuwa chini yetu msimu huu wata-perform zaidi, ina maana watatushusha!

Kama sikosei, sisi ndo tulifunga ule mstari wa nchi 12. Sasa kama ndivyo, halafu aliyekuwa 13, 14 au hata 15 waka-perform vibaya zaidi, basi tutasonga lakini kama #13 msimu huu aki-perform vizuri, lazima atatushusha manake nakumbuka hatukuwa tumemzidi point nyingi.

Itabidi nitafute ile standing ya mwaka jana nione uwezekano uliopo!
 
Ni kwamba aliyetuzidi point ambaye katupokonya hiyo nafasi amekuwa disqualified kushiriki mashindano yoyote ya CAF. so swali ni kwamba tutapanda sisi tunayefuatia?
Unajua kabla sijasoma hii post, post yangu ya mwisho nilikuwa nazungumzia kuitafuta ile standing ya msimu uliopita! Btw, ni nani huyo ambae alitupokonya nafasi?! Lakini kama unachosema ndicho kilichopo, basi tutapanda sisi
 
yote hayo nilisikia bado pointi zilitosha mwakani
Ni kwamba aliyetuzidi point ambaye katupokonya hiyo nafasi amekuwa disqualified kushiriki mashindano yoyote ya CAF. so swali ni kwamba tutapanda sisi tunayefuatia?
Ile ranking niliyokuwa naitafuta ni hii hapa chini:-

Kumbe aliyekuwa anatufuatia (Ivory Coast) tulimzidi point 3... hizi ni nyingi sana!

Good news ni kwamba, kuanzia Ivory Coast hadi Uganda hakuna hata mmoja aliyefika Group Stage ya CAF Champions... kwa maana nyingine, hawana additional points kutoka CAF Champions!

Zimbabwe ameingiza FC Platinum kwenye Group Stages lakini good news ni kwamba, mosi; anaburuza mkia kwenye kundi lao na pili, yupo chini sana kwenye msimamo... yaani kwenye previous ranking, yupo #20 huku ukiwa na point 8 TU!

FC Platinum hata ukitokea muujiza akapewa ushindi wa mezani wa CAF Champions, ina maana Zimbabwe watapata 6 Additional Points, so 8+6 = 14... bado hawatufikii!!!

Ukirudi kwenye CAF Confederation, Ivory Coast na Mali wameingiza timu moja moja kwenye Group Stage. Mali kwenye msimamo wa hapo juu wapo chini sana, na wanazo Points 3 TU! Meaning, Timu kutoka Mali hata ikichukua ubingwa wa Confederation CUP, watapata only 5 Points ambazo total itakuwa 8 points ambazo zipo chini sana!!

Kwa upande mwingine, mwakilishi wa Ivory Coast ambae ni FC San Pédro anaburuza mkia kwenye kundi lao! Kwa maana nyingine, na hatasonga mbele and in turn, no addiotional points kwa Ivory Coast!

Sikuzifanyia analysis timu za juu kwa sababu sioni ni namna gani wanaweza kubadilisha msimamo huku chini! Hivyo basi, msimu ujao ni Timu 2 x 2!!
 
Mkuu Yanga tulitetereka kidogo kwenye mechi mbili tatu, nakuhakikishia sasa hivi hatutafanya makosa tena.
Tunachukua kombe la ligi kuu Simba hawataamini macho yao.

Daima mbele
Labda mkachukue kombe kijijini kwenu huko namtumbo
 
Afu nimeona siku hizi mambo yote ya usajili na uendeshaji wa club huwa anazungumza yule Engineer wa GSM hivi ni kwamba Yanga hakuna uongozi au njaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…