Yanga kutupwa nje ya Azam Conf. Cup

Yanga kutupwa nje ya Azam Conf. Cup

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Dalili zipo wazi Yanga imetepeta mno,hata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ni shida.

Kwa upande wa Azam Conf. Cup Yanga watatolewa mapema .

Yanga tangu mechi ya march 8 kuifunga Simba ni kama imechanganyikiwa,Sijawahi kuona akili za kijinga hivi za wanayanga wameshindwa kufocus games zilizo mbele zao wanasherekea goli ya tar 8,wanafungwa kila siku lakini wamefocus tar 8 march badala ya mechi zijazo.

Simba wanachukua ubingwa wao wanashangilia mechi ya tar 8, azam conf Itachukuliwa pia wao bado wanashangilia bao la march 8 ,hizi ni akili au matope?
Halafu hiyo mentality ikawaingia hadi viongozi wao na wachezaji kwamba kumfunga simba wamemaliza ligi.

Mmebakiwa na azam conf. Cup endeleeni kushangilia march 8,Kimataifa mtasikilizia kwa wengine
 
Mkuu Yanga tulitetereka kidogo kwenye mechi mbili tatu, nakuhakikishia sasa hivi hatutafanya makosa tena.
Tunachukua kombe la ligi kuu Simba hawataamini macho yao.

Daima mbele
Labda siyo ligi ya bongo,sasa hivi simba akitoa hata dro mbili anachukua kombe
 
Simba, kimataifa kwenyewe mnakwenda kutolewa tena, kwenye stage ya awali ya 'mchujo' na Muzinga Fc ya Burundi alafu mnarudia kwenye kale ka mchezo kenu tena ka- kuhongo marefa na kununua mechi kama ilivyo kuwa msimu huu
 
Yanga wanajua hawana cha ku-gain wala ku-lose kwenye VPL! Kinyume chake, kwenye Azam Confederation Cup, huko wanacho cha ku-gain, na kukosa kwake, ni ku-lose; na kwahiyo lazima wapigane Jihad!
 
na nye nendeni kimataifa ,siyo mnasherekea dro
 
Yanga wanajua hawana cha ku-gain wala ku-lose kwenye VPL! Kinyume chake, kwenye Azam Confederation Cup, huko wanacho cha ku-gain, na kukosa kwake, ni ku-lose; na kwahiyo lazima wapigane Jihad!
ila hizi mechi za vpl ndo kipimo tosha
 
ila hizi mechi za vpl ndo kipimo tosha
Ligi yoyote bingwa akishajulikana tu tayari inakosa msisimko hasa ukizingatia nafasi ya 2 na 3 hazina faida yoyote! Ingekuwa kama zamani kwamba 3 Bora wanaenda Ligi ya Muungano, bado kipute kingekuwa kikali!
 
nafasi ya pili ina umuhimu,iwapo ikitokea simba akichukua vpl na azam cup,wa pili kwenye msimamo wa ligi ndo atakayeenda kimataifa
 
nafasi ya pili ina umuhimu,iwapo ikitokea simba akichukua vpl na azam cup,wa pili kwenye msimamo wa ligi ndo atakayeenda kimataifa
Kwanini aende wa pili kutoka VPL wakati huko kwenye Azam Confederation na kwenyewe kuna mshindi wa pili?!
 
Kwanini aende wa pili kutoka VPL wakati huko kwenye Azam Confederation na kwenyewe kuna mshindi wa pili?!
mkuu if im not wrong navyojua mshindi wa pili anakuwaga kutoka azam cup au mtu wa pili kwenye msimamo wa vpl iwapo timu moja itachukua kombe zote
 
Simba na Yanga wakishinda watakutana Nusu Fainali, sio Fainali.

Yeah maana simba na azam atakayeshinda anakutana nusu fainali na mshindi kati ya yanga na kagera sugar
 
mkuu if im not wrong navyojua mshindi wa pili anakuwaga kutoka azam cup au mtu wa pili kwenye msimamo wa vpl iwapo timu moja itachukua kombe zote
Baada ya hoja yako hii nikalazimika kujiuliza ilikuaje KMC walishiriki Kombe la Shirikisho na sio Lipuli ambao walishika namba 2!!

Nilichogundua, kama kawaida yetu huwa hatuna plans for future! Baada ya msimu uliopita kuwa na nafasi 4 (2 Mabingwa, na 2 Shirikisho), hiyo kwetu ilikuwa ni surprise ambayo haikuwa documented earlier just in case inapotokea issue kama hiyo!!

Kutokana na hilo, TFF wakalazimika kubadili kanuni na kuweka Mshindi wa 1 & 2 VPL aende Club Bingwa na Mshindi #3 aende Shrikisho kama Mwakilishi #2 baada ya Mshindi!

Kule Azam Cup, Mshindi alikuwa Azam na #2 alikuwa Lipuli, na VPL #3 alikuwa Azam. Kwa maana nyingine, kwavile Azam alikuwa huku na huku, ndipo akachukuliwa KMC aliyekuwa VPL #4!

Swali ninalojiuliza ni: Hivi namba 2 kule Azam Cup angekuwa Yanga, wakati VPL angekuwa #5... hivi kweli TFF wangesema #3 VPL ndo aende Confederation Cup na kumchinjia baharini Yanga aliyekuwa #2 kwenye Azam Cup?!

Hii kanuni waliifanyia roho mbaya Lipuli kwa sababu hawana wa kuwatetea!!!

Sasa kama kanuni mpya ilikuwa fixed kwamba Mshindi wa 3 ndie aende Confederation na sio mshindi wa pili au watakaofuatia, basi utaibuka mgogoro mwingine wa kikanuni kwa sababu kama Azam atakuwa #2 VPL huwezi kumruka halafu aende Yanga au Namungo unless kama yeye awe ndo bingwa wa Azam Cup!!

Na akishakuwa bingwa, ina maana #2 ya VPL itakuwa useless!

Lakini kama kanuni inatamka bayana kwamba #2, au #3 au #4 n.k atawakilisha CAF in case Simba anakuwa bingwa Azam Cup, then ligi bado inaendelea kwa sababu both Azam, Yanga na hata Namungo wataendelea kuvutiwa na VPL #2.
 
Back
Top Bottom