Yanga Lives Matters

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Your browser is not able to display this video.


Mashabiki wa Yanga wakipaza sauti hawamtaki Yikpe.

Hii sio sawa kabisa. Mngevumilia ligi iishe muone usajili mpya. Mnawatisha wachezaji hata nafasi ya pili mtakoss

#Icantbreath
#YangaLivesMatters
 
Tatizo la Yanga katika suala la usajili, ni sawa na tatizo la mtoto mchanga kujikojolea. Wavute tu subira
 
ila pale hakuna mchezaji, ni sawa na nyau walipo msajili linno musombo.
 
Na timu ametoa rasmi tamko kwamba mashabiki zao wasiwatukane wachezaji na kuwatishia,pia wasigombane wao kwa wao
 
Mi sioni tatizo la kina Yikpe wala Molinga.
Wanachokosea mashabiki wanawavalisha hawa jamaa viatu vya Makambo na wakati huohuo wanasahau kuwa hawana viungo wakupiga Pasi za mwisho...Haruna Nyonzima no udambwiudambwi tu hapigi pasi mujarab kwenda kwa wafungaji...kifupi MTU Huyo
hayupo pale yanga kwa sasa alikua Ajib msimu uliopita.
Nafasi hata Kagere anakosa sana tu...lakini anapata nyingi ndo mana anafunga.
sasa unamuandama Molinga mwenye goli 8 hapo Yanga wakati chilwa yupo na kina Sureboy pia ana goli hizohizo naye wasemaje?
Yanga watafute kiungo mpiga pasi za mwisho siyo mpanda mipira na Huyo mwingine mpiga back passes halafu mnalaumu strikers...and in case they don't Nchimbi amefunga magoli mengi alipokua Police kuliko hapo yanga msimu huu.
Balama mapinduzi ye mbio tu..ubunifu hakuna.
Na hii siyo disrespect kwa yanga huu ni ukweli.
 
Kagere ana magoli mangapi ya offside na penalty za uzushi
 
Wakulaumiwa ni hao hao mashabiki wenyewe vichwa panzi kabisa. Yaani wanasahau haraka sana. Mkwasa alikataa Yikpe asisajiliwe mpaka afanye majaribio amuone. Akaondoka na timu akaenda zake Mbeya. Huku nyuma mashabiki hao hao wakashinikiza Yikpe asajiliwe. Na uongozi kwa kuogopa shinikizo wakamsajili fasta bila majaribio wakamsafirisha kwa mbwembwe kwenda Mbeya. Leo tena wamegeuka wamesahau kuwa shinikizo lao kwa uongozi ndio lililosababisha dhahama yote hiyo.

Na Yikpe bonge la mjanja alijijua ndio maana akagomea majaribio. Sasa uongozi ndio utakaopata hasara kwa kuvunja mkataba na Yikpe labda tu kimsingi watumie busara wakae nae chini wamuombe kiungwana akubali kupunguza gharama za kuvunja mkataba. "Next time" braza Msola na mwenzio Mwakalebela msifanya maamuzi kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki maana mambo yakienda ndivyo sivyo hao hao wanawageuka fasta.

Daa ila haya mambo ya mpira wakati mwingine yanachanganya sana na hayatabiriki kabisa, yaani unamuacha Balinya halafu unamsajili Yikpe.
 
Sidhani kama nimeongelea offside goals hapa wala penalty za uzushi...kifupi sipo kuelezea ubishani wa Simba na Yanga.
Ok magoli mangapi halali ya Yanga yanakataliwa toka msimu uliopita na penalty halali..Msomali anafikiria Malinzi alikuwa anaibeba Yanga analipizia Msuva Tambwe na Ngoma walikuwa hatari sana ..nakumbuka mechi na Prison Mbeya Kakolanya alidaka penalty..lini Simba wamepigiwa penalty wakati makosa ni mengi wanafanya ..double standard
 
Nakueleza sipo hapa kubishana kuhusu Simba na Yanga mbona hunielewi? uliza swali kwenye nilichoongelea utajibiwa kinyume na hapo sitajibu chochote.
 
Kwa mashabiki nyie mpira wa bongo hautakaa ufike popote, huyo yikpe mkimvunjia mkataba ataondoka je gharama za kuvunja mkataba mpo tayari kuzibeba? Sio mambo ya kuvunja mkataba muanze janjajanja ya kumlipa, nikirudi kwa ulichochangia ni hisia tu wala hakuna kubebana ila kuna tatizo la kiwango duni cha waamuzi
 
Well said!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…