Yanga mbovu yatoka suluhu na TP Lindanda Pamba SC

Daaa hiki kikosi hiki kimeanza kunipa wasi wasi
 
Mimi ni yanga ila bado sijajua mpaka sasa pale Yanga tatizo ni wachezaji au kocha maana sioni wanachofamya uwanjani zaidi ya kubutuabutua ila Balama bonge la mchezaji ila amekosa wakucheza na tu
 
Hvi Yule striker aliyefunga bao la kusawazisha ana miaka mingap kweli ?? Nahsi kama ana 40+
 
Ni washabiki wa timu fulani pekee ndio: 1. Wanaoshindwa kutofautisha baina ya kikosi kamili na kikosi cha kwanza, na ya kikosi cha kwanza na kikosi cha kwanza kamili 2. Wanaoitikia bila vinanda wimbo wa wanatimu wenzao ndani ya TFF wa kuhusisha mavazi nadhifu na benchi la ufundi hata kabla ya kujua maana ya neno ‘nadhifu’ 3. Wanaodhani ufundi mpirani ni kucheza mpira badala ya kucheza ushindi 4. Wasiojua kwamba timu ndogo kama Pamba ndiyo inakuwa na ari zaidi ya ushindi inapocheza na timu kubwa kama Yanga, kwamba timu inapocheza na upungufu wa mchezaji ndiyo inakuwa na motisha zaidi wa kucheza kwa nguvu, na kwamba wachezaji wenye mechi muhimu zaidi usoni hukosa ari ya kucheza jihadi kwenye mechi za maandalizi 5. Wanoichukia Yanga kiasi cha kujikuta wakidanganya kuwa wako Mwanza ilhali wanaendelea na mishemishe zao za kawaida mitaani mwao 6. Kama kweli wako Mwanza, wanaofanya kisebusebu cha kuichukia Yanga kumbe hawajiwezi mpaka wakaione ikicheza. 7. Wanaoshindwa kujua kwamba mechi ya kirafiki ikimalizika salama bila ya timu yenye mashindano makubwa usoni kupata majeruhi basi wapenzi wake wanapaswa kuungana na benchi lao la ufundi kufurahia hali hiyo bila ya kujali matokeo ya mechi yenyewe 8. Wanaosahau kwamba hata Yanga ikifungwa mechi zote za kirafiki, kimataifa na za ligi, matokeo hayo hayatafuta ukweli kwamba timu yao wanayoiona ndio bora duniani bado itabaki kuwa imetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye raundi ya kwanza.
 
Vipi Viongozi,Kocha na watazamaji walivaa vipensi?
 
Haujaandika kama mwanamichezo, umeandika kama mpenzi wa Mikia Fc.
 
Kocha wao amekalia kuvaa vipensi atakua na undugu na Ali Kiba.
 
Acha ubishi mwaka huu hatuna timu hata tuongee vipi timu yetu ni mbovu
 
Mikia FC buana.
 
Ile papa mauji kipande ya mtu Molinga embu mshaurini apunguze ule mwili, jana alikuwa anarukaruka tu uwanjani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…