Yanga Mchukueni Hashim Mbaga Kulipa Kisasi

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Wakuu Kwema?

Kwa sasa tuko kwenye usajili, ndio msimu wake huu. Simba walimsajili aliekua Mchezaji wa Yanga Bernad Morrison. Yanga "wakalipa" kwa kumchukua aliekua CEO wa Simba bwana Senzo Masingiza Mbatha.

Sasa Simba wamechukua Mchezaji aliekua akiwaniwa na Yanga Mzambia Larry Bwalya. Ushauri wangu wa Yanga ni kuendelea kuchukua kiongozi wa Simba. Kuna huyu Mkurugenzi wa Wanachama wa Simba Bw. Hashimu Mbaga.

Huyu Ni Chanda na Pete na Senzo, hata kusimamishwa kwake ingawa hakuwekwi wazi ila ni sababu ya urafiki wake na Senzo. Huyu hata ofisi alikua akitumia moja na Senzo.

Yeye ndie aliekua akimtafutia Senzo mademu, kumtafsiria meseji mbalimbali za Kiswahili za Twitter, Instagram pia kumsaidia kuzijibu. Habari hizi nimezipata kwa Jamaa wa karibu wa Hashimu ambae tunakutanaga tunapataga Lager pamoja.

Sasa basi Yanga ikimchukua huyu itakua imelamba dume. Tofauti na Senzo ambae hakua Mwanachama, Mshabiki wala Mpenzi wa Simba hapo kabla ya kuja Simba, huyu Hashimu yeye ni Mpenzi, Mwanachama na Mshabiki wa Simba, hivyo Yanga wakiweza kumfanya abadili timu watakua wamelamba dume.

Kifupi mchezo utakua Simba inasajili Wachezaji wanaowaniwa na Yanga wakati Yanga inasajili waliokua Viongozi wa Simba.
 
Yule mzungu hakukosea kwa kweli kuwaita MANYANI. Huyo na senzo wanacheza no zp?
 
Dah!

Ulitabiri na kwasasa yupo ananyia debe.
 
Baada ya kutoka taarifa za aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki Simba, Hashim Mbaga kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kudhaniwa anawahujumu waajiri wake wa zamani, bado kulikuwa na maswali mengi kuhusu kukamatwa kwake.

Baada ya kufanya utafiti wa kina, kutoka kwa vyanzo kadhaa, hatimaye nimepata chanzo cha kushikiliwa kwakwe na Jeshi la Polisi.

Kuna mawasiliano ya Mbaga na Senzo yamenaswa [WhatsApp] ambapo wawili hao walikuwa wakijadiliana kuhusu Mbaga kwenda Sumbawanga na kuna jambo ambalo alitakiwa kwenda kulitekeleza akiwa huko.

Katika majadiliano yao, Bw. Senzo aliahidi atatoa kiasi cha pesa kwa ajili ya kugharamia safari ya Mbaga (kwa ndege) kwenda Sumbawanga na kurudi Dar.

Kwa mujibu wa majadiliano yao, inaonekana mpango wao haukuwa Sumbawanga pekee, baada ya kurudi Dar Mbaga alitakiwa kuendelea na jambo lao hadi timu itakapotudi Dar na itakapoingia kambini kwa kujiandaa na mechi ya WATANI WA JADI!

Maswali ya kujiuliza:

1. Wawili hawa walikuwa na mpango gani na Simba kule Sumbawanga? Hashim Mbaga kwa sasa sio kiongozi tena wa Simba, Senzo ameshahama Simba yupo Yanga.

2. Je, Senzo alikuwa anamtumia Mbaga kuihujumu Simba kwa sababu waliwahi kufanya kazi pamoja?

3. Kwa nini Senzo analipa gharama za safari ya Mbaga kwenda kwenye mechi ya Simba wakati yeye sasa kwa sasa yupo Yanga?

Haya mambo ya kuhujumiana na kutafuta matokeo nje ya uwanja hayana afya kwenye soka, kila timu itafute na kupata matokeo uwanjani kutokana na maandalizi iliyofanya
 
Mkuu Heshima kwako. I think this is too low to you.
 
aya mambo ya kuhujumiana na kutafuta matokeo nje ya uwanja hayana afya kwenye soka, kila timu itafute na kupata matokeo uwanjani kutokana na maandalizi iliyofanya
Yapo toka zamani. Na siyo kosa kuwaahidi wachezaji wa timu pinzani hela wakiifunga Simba/Yanga. Ila ni rushwa kutoa hela kwa wachezaji ili wasicheze vizuri au waamuzi ili wasitoe haki.
All in all, mwaka huu hautakuwa rahisi kwa Simba kuchukua ubingwa. Bado channels zipo nyingi sana, labda tu kama hujui mambo ya mpira.
 
Shafii Dauda
 
Leo tarehe 02/11/2020 nimemsikia kiongozi mwenye ushawishi mkubwa Simba ndugu Hans pop kwenye kipindi cha michezo pale EFM na nikatafakari na matamko ya kiongozi mkubwa wa Simba MO Dewji, kwanamna nilivyo Yapima mazumgumzo yao nimegundua mashabiki wa Simba wana matarajio makubwa na timu yao ila viongozi wanao tegemewa kwenda kuyatafsiri matarajio ayo ya wapenzi wa Simba wana operate kwa kiwango na uelewa mdogo sana katika soka la kisasa.

Sasa napata picha aliyekua kiongozi wa Simba miaka ya nyuma Ismail Aden Lage anaujua mpira vizuri kuliko viongozi karibu wote walio madarakani kwasasa mwaka 2020.Sasa nimepata picha kulingana na uelewa wa viongozi wa Simba waliopo sasa Hakuna mabadiliko yoyote ya maana yanayoweza kuletwa na uongozi uliopo sasa ni swala la muda tu tuta elewana.
 
Unadhani Senzo hakusoma darasani, kwamba anaujua tu mpira?
Maana Yangu sio kila aliye soma uongozi anaweza kuongoza mpira miguu wa kisasa, mpira wa miguu wa kisasa wa kibiashara unaendeshwa tofauti kabisa na uongozi wa taasisi nyingine ambazo haziusishi michezo.
 
Maana Yangu sio kila aliye soma uongozi anaweza kuongoza mpira miguu wa kisasa, mpira wa miguu wa kisasa wa kibiashara unaendeshwa tofauti kabisa na uongozi wa taasisi nyingine ambazo haziusishi michezo.
Syllabus ya Management inafanana karibu kote duniani, sana sana kama inaweza ikaongezeka course inayoendana na unachotaka kuongoza. Management is both science and art, kwamba kuna mambo yanabaki kama principle ilivyo (science) na mengine unajiongeza kwa ubunifu wako (art).Kwa hiyo si kweli kwamba uongozi wa mpira una tofauti na uongozi wa sector nyingine, ni kuji.tune tu
 
Uongozi siyo management.
Ila management ni sehemu ya tu ya uongozi (administration).
Kwa hiyo kwa kuanzia tu, kimantiki hujaelewa alichosema uliyemnukuu.
Mimi nakubaliana na uliyemnukuu based on interview ya jana, jamaa wanaoneka ni weupe.
 
Uongozi siyo management.
Ila management ni sehemu ya tu ya uongozi (administration).
Kwa hiyo kwa kuanzia tu, kimantiki hujaelewa alichosema uliyemnukuu.
Mimi nakubaliana na uliyemnukuu based on interview ya jana, jamaa wanaoneka ni weupe.
Kumsaidia huyo jamaa ndio maana Tff imehamua kuanzisha kodi za uongozi wa mpira ili kupata viongozi halisi wa mpira na sio wale waliosomea business administration.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…