Kwanza nachukua fursa hii kuwapongeza Yanga pamoja na kwamba kwenye haya mashindano karibia timu zote zilizoshiriki zina hali mbaya ya kushuka daraja kwenye ligi zao.
Sio kwamba mmepata mafanikio haya kwa kuwa mna wachezaji wazuri sana hapana, bali ni kujituma kwao ndio kumeleta mafanikio haya tofauti na pale Simba mchezaji hata akiwa mzuri kiasi gani akishafunga kagoli kamoja ajiona hakuna kama yeye, hasa kushinda ugenini ni kazi kweli kweli pale Simba.
Mpira wa miguu una mambo mengi mfano kucheza na kumiliki mpira na kuwalamba watu chenga bila kufungua au kushinda mechi hakuna heshima hapo kama yanayofanyika pale Simba. Ona butua butua za Yanga zinawapeleleka Fainali hata hata kama za 'malosers'. Fainali ni Fainali, hongereni sana na mmeiheshimisha nchi.
Pia Yanga mnastahili pongezi kwa kudumisha demokrasia ya kuwakosoa viongozi na hata wawekezaji wenu pale wanapokosea. Hii inawasaidia sana kuweka mambo sawa tofauti na pale Simba ukiulizia tu ziko wapi billion 20 za mwekezaji unaaza kutukanwa na kuitwa wewe ni Yanga.
Au ukisema baadhi wachezaji muhimu kama Manula, Chama, Inonga, Baleke na Mzamiru wameshuka viwango unaanza kuitwa kuwa wewe ni Yanga. Au ukisema kulikuwa hakuna sababu ya kuwapumzisha wachezaji muhimu kwenye mechi ya Namungo iliyopekea kukosa kwao match fitness na kufungwa na Azam kwenye FA utaambiwa wewe ni Yanga.
Mwisho pamoja na kwamba kuna mambo Yanga wanejifunza kutoka kwa Simba lakini bado Simba wanayo mengi zaidi ya kujifunza kutoka kwa Yanga kwa mafanikio haya ya ghafla waliyofikia.