Yanga mmezidi na mnatia aibu

Singasinga

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2011
Posts
2,711
Reaction score
3,279
Habari wanajukwaa

Nikiwa kama mdau wa soka la nchi hii nasikitishwa sana na tabia isiyokoma ya Viongozi wa yanga kuamini ushirikina na vurugu za kuvunja mageti na kupita milango isiyoruhusiwa kama njia ya kupata ushindi team inapocheza

Najua Faini mnazopigwa ni ndogo sana kwenu ndio maana kila mara imekua ndio kawaida yenu tangu msimu uliopita hadi jana.

Badilikeni sana la Sivyo hata mkichukua kombe mtachukua mkiwa mmechoka sana hata nguvu ya kulinyenyua kombe hazitakuepo.

No Comfortable win at all,shame on u[emoji34]

Mna kikosi kizuri sana ila mmeshaathirika na punyeto ya kifikra,
 
Mmesahau nini nyie nyau fc?
 
Nyie mbona mliajiri paka mlikuwa mnawafanyia kazi gani labda waeleze wanajukwaa waelewe nini kazi ya paka mpirani!
 
ni aibu wameajili rundo la makocha lakini bado wanaamini ushirikina kama kweli unafanya kazi mbona hawakuutumia Nigeria wakapigwa nje ndani.
Kati yaYanga na simba, ni timu gani ina lundo la makocha? Yanga ina makocha wawili ! Nabi na Msaidizi wake Kaze. Huku Mwinyi Zahera akipewa nafasi ya mtaalamu wa ufundi kwa timu ya vijana.

Huku timu yako ya simba ikiwa na makocha watatu! Kocha Mkuu (sasa hapa sijui ni huyu Ngumbalu/Memkwa wenu Gomez, au yule Thierry Hitimana) na Msaidizi Suleiman Matola! Jumla watatu.
 
tatizo ni kwanini hamuwaamini makocha wenu kila siku mtakuwa mnapigwa faini ya kuendeleza vitendo vya ushirikina
 
Kwani shida nini au mayele ? Ni ushamba kuamini unaakili kubwa kumbe ni makolokolo tu.

Mechi na platnum yule paka alikiwa wa nini?

Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
Ni aibu viongozi, benchi la ufundi na wachezaji kukaa na kupanga kutopita geti rasmi.Maana yake klabu inakuwa imeweka ushahidi hadharani kuwa inaamini ushirikina. Ila kwa shabiki kushikilia nyau au kunguru hakuna ushahidi kuwa ushirikina anaofanya katumwa na klabu.
 
Word
 
Huu ujinga sio kwa yanga tu, ni karibia timu zote tu za Tz, na hili wa kulaumiwa ni TFF, na bodi ya ligi tu ndio wanalea huo ujinga, kwa kuweka faini ndogo!!mfano wakiweka kanuni kuwa timu yoyote itakapoingia uwanjani kwa kutumia mlango/geti lisiloruhusiwa adhabu yake watapokonywa alama 3, na magoli matatu, unafikiria huo ujinga utaendelea?lakini kwasababu hao hao viongozi nao wanaamini huko huko ndio maana huu ujinga hauwezi kuisha.
 
Ushirikina hauna nafasi katika mchezo wa soka, tuache upumbavu hakuna uchawi unaweza ukafanya eti ushinde mechi zote wakati una timu mbovu, hilo halipo.

Hii dhana ya ushirikina inayotumiwa na vilabu fulani nafikiri ni njia tu ya watu kupiga pesa huku wakifahamu vizuri nini wanachokifanya. Ingekuwa kweli wasingetumia pesa nyingi kuwalipa mishahara makocha, wangeziokoa basi hizo pesa.
 
Makolo Muli Bwanji Kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…