Yanga mnaivimbia TFF kisa kanuni imekiukwa. Mmejipanga kuzifuata kanuni zote au ni mihemko tu?

Wagawane point tena tatu tatu
 
Huyo Msomali atashindwa uchaguzi ujao na TFF mpya itapatikana, TFF ya sasa haina maslahi yoyote kwa Yanga. Tena wawaambie watu namna ya kurudisha viingilio vyao.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Hapo kinachoongelewa ni kuhairisha mchezo na sio mda wa mchezo boss
 
Kwenye ile barua waliyotoa jana TFF hiyo sababu iliwekwa? Kuwa muelewa ndugu,Fifa inaruhusu serikali kuingilia kama kutakuwa na usalama mdogo yaani polisi au mamlakani ya hali ya hewa wakitangaza kutatokea na hali mbaya.
Sasa barua ya hao TFF ilisema sababu ya kusogeza mchezo mbele kwa masaa mawili?
Saa 11 usalama ulikuwa mdogo uwanjani? Je Yanga na Simba ziliambiwa sababu hiyo?
Hali ya hewa ilikuwa mbaya saa11? Je Yanga na simba waliambiwa?

TFF imeshikwa pabaya safari hii na yanga, kama wanauwezo wawapige faini yanga kwa kutotii maagizo yao ya hovyo. Kisha Yanga wapeleke malalamiko yao FIFA ndipo utaelewa
 
Yanga hawajaigomea tff wameigomea serikali bahati mbaya yao wamefanya uamuzi kwa kukurupuka wakidhani wanawakomoa TFF. tnaenda kuona gsm wakiyumbishwa mpaka waombe poo.
Serikali na mpira wa miguu wapi na wapi? Kama wao wababe wakipokea pointi yanga na mengineyo kama wanauwezo huo
 
Kanuni imesema timu iambiwe sababu ya kuahilisha mchezo?

Kanuni imeipa TFF kutafsiri sababu kama ni dharura na msingi siyo timu na TFF.

Serikali haikutoa maamuzi na haijaingilia mchezo bali ilitoa taarifa kwa TFF na TFF walifanya maamuzi baada ya kutafakari yaliyotoka serikalini. TFF hawajashinikizwa na yeyote na hapo unaiingizaje suala la katazo la FIFA la serikali kutoingilia michezo?

Mbona mechi ya jana ya Namungo ilisogezwa na wakacheza? Mbona mechi ya jana ya Yanga princess ilisogezwa na wakacheza?

Ukweli ni kuwa watu hawakusoma vifungu kwa ujumuishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…