Yanga, mnapowapokea wageni kumbukeni na kuwasindikiza

mpiga vichwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
2,376
Reaction score
3,811
Ni jambo zuri na la kiungwana kabisa pale utakaposikia mgeni atakuja kwa jirani yako wewe unafanya maandalizi ya kwenda kumpokea stendi au uwanja wa ndege bila hata kupata rukhusa ya jirani yako pengine hata nauli hauna lakini unakopa ili ukampokee na kumsindikiza hadi kwa mwenyeji wake. Ni jambo zuri kwakweli.

Lakini huo uungwana unakuwa hauna Maana tena pale yule mgeni anapokwambia nataka kuoondoka naomba unisindikize we unamchungulia dirishani huku anaangaika na mabegi yake hadi uwanja wa ndege. Watoto wa mjini wanasema kumsagia kunguni.

Ukipokea , kumbuka na kusindikiza.
 
Msitupangie ya kufanya.
 
Kaizer Chiefs nao wasindikize wageni wao Al Ahly [emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…