Yanga msione aibu ni wakati muafaka kutembeza bakuli

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Kwa kinachoendelea pale jangwani ni wazi hali ni tete, sote tunajua hali ya upepo kila kukicha inazidi kuharibika mifuko inazidi kukauka. Wafadhiri wakubwa pamoja na mapedejee hali zao ki uchumi zimeyumba sana ndani ya miaka miwili hii Yanga sports club ni wakati wa kuwageukia mashabiki wenu mmoja mmoja mwenye uwezo wa kuchangia afanye hivyo

Ni ushauri wangu tu kwenu zitangazeni namba zenu halali za M pesa Tigo Pesa na Airtel Money wakereketwa wenu waokoe jahazi hili, wakijitokeza mashabiki milioni 10 wakachanga japo1000 tu hakika zitawasogeza sana, vinginevyo mnakwenda shuka daraja
Huo ni ushauri tu, hata simba mjue hao wanaowapa support nao watachoka si mbali, chukueni hatua ukiona mwenzio ananyolewa...

Otherwise baada ya miaka miwili tutegemee mabadiliko makubwa kwani tutabakiwa na Jkt Ruvu, Tz Prison na Azam tu Ligi KuuYaVodacom
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…