Yanga msitafute mfungaji bora wa ligi

Yanga msitafute mfungaji bora wa ligi

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Wacha mfungaji bora ajitokeze tu by chance na sio kulazimisha lazima mfungaji bora atoke Yanga. Kufanya hivyo kutakuwa na athari kadhaa zikiwemo:

1. Kumchosha mchezaji mmoja huyohuyo ambae mnamtaka awe mfungaji bora kwenye ligi. mtamlazimisha kumchezesha mechi zooote za ligi.

2. mchezaji huyo anakuwa na hofu ya kupitwa kwenye ushindani na kusababisha kukosa kufunga hata magoli ya wazi.

3. Baadhi ya wachezaji wenzake kwenye kikosini wanaweza kuacha kumpa ushirikiano

4. Mchezaji huyo utakamiwa sana na wachezaji wa timu pinzani

5. Timu yenu inaweza kukosa kupata magoli mengi au point 3 kwenye kila mechi.

6. Wachezaji wengine kwenye timu watakata tamaa.

Waacheni magoli ya aina mbalimbali yafungwe na wachezaji wa aina mbalimbali kwenye timu, hatimae Yanga inashinda kama timu.
 
Unazungumzia Ile penalty sio?
Sio penati tu, hata free kicks, hata kumpumzisha kabisa mchezaji kwenye mechi ili apate nguvu zaidi na muda wa kupona lakini kuwapa nafasi na wachezaji wengine. Timu inayoshinda haibadiliki wanasema, lakini kama mchezaji anachezeshwa, anapewa kupiga penati au free kick ili timu ipate matokeo ni sawa, lakini kama anachezeshwa na kupewa kupiga penati au free kick ili tu aongeze idadi ya magoli yake sio sawa. Mfano, wachezaji bora wa kupiga free kicks lazima watambuliwe na wapewe hiyo kazi.
 
Naunga mkono hoja. Ifikie wakati Yanga wawekeze nguvu kubwa kwenye kupata pointi 3 muhimu.
Kumbebesha majukumu mengi Fiston Mayele, kutamuongezea tu fatique kabla hata msimu wa ligi kuisha.

Lakini pia waache kumpa majukumu ya kupiga penati. Yanga ina wapiga penati wengi! Mfano Juma Shabani, Dickson Job, Yannick Bangala, nk.

Ningeshangaa sana kama angefunga ile penati kwenye mechi na Polisi!
 
Ningeshangaa sana kama angefunga ile penati kwenye mechi na Polis
Sio afya kwa wachezaji wenzake, mashabiki, uongozi, na hata kocha mwenyewe mchezaji kupoteza penati kwa kigezo cha kuongeza idadi binafsi ya kuongeza magoli yake. Kila mtu akiwa kwenye nafasi ya kufunga afunge badala ya kupasia mtu afunge hata kama hayuko kwenye nafasi nzuri ya kufunga.
 
Naunga mkono hoja. Ifikie wakati Yanga wawekeze nguvu kubwa kwenye kupata pointi 3 muhimu.
Kumbebesha majukumu mengi Fiston Mayele, kutamuongezea tu fatique kabla hata msimu wa ligi kuisha.

Lakini pia waache kumpa majukumu ya kupiga penati. Yanga ina wapiga penati wengi! Mfano Juma Shabani, Dickson Job, Yannick Bangala, nk.

Ningeshangaa sana kama angefunga ile penati kwenye mechi na Polisi!
NI SAWA MKUU
 
inategemea mkuu na plan za timu kwa msimu husika, uko sawa chief
Penati na free kicks hazina mwenyewe, hata wachezaji wakubwa wanazikosaga pia, lakini hii haimaanishi wapigaji wazuri wa faulu hawafahamiki
 
Utopolo akili hawana
Wacha mfungaji bora ajitokeze tu by chance na sio kulazimisha lazima mfungaji bora atoke Yanga. Kufanya hivyo kutakuwa na athari kadhaa zikiwemo:
1. Kumchosha mchezaji mmoja huyohuyo ambae mnamtaka awe mfungaji bora kwenye ligi. mtamlazimisha kumchezesha mechi zooote za ligi.

2. mchezaji huyo anakuwa na hofu ya kupitwa kwenye ushindani na kusababisha kukosa kufunga hata magoli ya wazi.

3. Baadhi ya wachezaji wenzake kwenye kikosini wanaweza kuacha kumpa ushirikiano

4. Mchezaji huyo utakamiwa sana na wachezaji wa timu pinzani

5. Timu yenu inaweza kukosa kupata magoli mengi au point 3 kwenye kila mechi.

6. Wachezaji wengine kwenye timu watakata tamaa.

Waacheni magoli ya aina mbalimbali yafungwe na wachezaji wa aina mbalimbali kwenye timu, hatimae Yanga inashinda kama timu.
 
Inabd wajue kuwa mfungaji bora haji kwa kufosi mnampa presha kubwa sana...cha muhimu ni alama tatu na magoli mengi coz hii ligi ya sahz ukipitwa goli moja tu tunakusahau..sasa endeleeni kumchosha braza mayele kwa kumpa tuta akati hawezi kupiga
 
Penati na free kicks hazina mwenyewe, hata wachezaji wakubwa wanazikosaga pia, lakini hii haimaanishi wapigaji wazuri wa faulu hawafahamiki

BIG NO..penati zina ufundi wake lini uliona djuma shaban au job wanakosa tuta?
 
Inabd wajue kuwa mfungaji bora haji kwa kufosi mnampa presha kubwa sana...cha muhimu ni alama tatu na magoli mengi coz hii ligi ya sahz ukipitwa goli moja tu tunakusahau..sasa endeleeni kumchosha braza mayele kwa kumpa tuta akati hawezi kupiga
ukitaka afanye vizuri ni apate muda pia wa kupunzishwa, sio hii ya back to back mechi 30.
 
Naunga mkono hoja. Ifikie wakati Yanga wawekeze nguvu kubwa kwenye kupata pointi 3 muhimu.
Kumbebesha majukumu mengi Fiston Mayele, kutamuongezea tu fatique kabla hata msimu wa ligi kuisha.

Lakini pia waache kumpa majukumu ya kupiga penati. Yanga ina wapiga penati wengi! Mfano Juma Shabani, Dickson Job, Yannick Bangala, nk.

Ningeshangaa sana kama angefunga ile penati kwenye mechi na Polisi!
Nadhani hilo suala lipo kwa Fiston mwenyewe wala sio timu kama ulishuhuhudia lile tukio baada ya penalty kutokea Mayele alikuwa wa kwanza kuukimbilia mpira na kuuweka kwapani akisubiri kupiga penalty

Nadhani Mayele ana presha kubwa na kiatu cha ufungaji bora ukizingatia hajawahi chukua kwenye maisha yake yoye ya soka na mimi naona ni jambo zuri kwa mchezaji kutamani mafanikio zaidi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka sana.
 
Nadhani hilo suala lipo kwa Fiston mwenyewe wala sio timu kama ulishuhuhudia lile tukio baada ya penalty kutokea Mayele alikuwa wa kwanza kuukimbilia mpira na kuuweka kwapani akisubiri kupiga penalty

Nadhani Mayele ana presha kubwa na kiatu cha ufungaji bora ukizingatia hajawahi chukua kwenye maisha yake yoye ya soka na mimi naona ni jambo zuri kwa mchezaji kutamani mafanikio zaidi
Si hivyo tu, lakiñi Mayele anajiona kama mtu mwenye deni kuuuubwa kwa watanzania wapenda Yanga kama asipofunga goli kwenye mechi. Hii inasababishwa na kupokelewa vizuri na watu Ile style yake ya ushangiliaji ya kutetema. Analazimika kutaka kufunga kwaajili Yao.
 
Nje ya mada we utopolo,endeleen kulazimisha kila mechi lazima then mtapata majibu tu,mana uto mmeambukiza mpaka wachezaji wenu kutokuwa na akili.
Eti wanamwacha apige penati ili akifunga watikikise matiti yao,shem on them
kuwasha moto uwanjani kupata matokeo ni akili?
 
Back
Top Bottom