Yanga na Simba ni za kawaida sana msimu huu

canfi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2022
Posts
1,368
Reaction score
1,477
Hizi timu ni za kawaida sana. Zimekuwa zikifanya makosa mengi sana kwenye michezo yao, kinachowaokoa ni udhaifu wa wapinzani. Sitashangaa hata Yanga ikipoteza mechi hivi karibuni.

Yanga inashinda kiujanja ujanja na kwa kutegemea wachezaji wachache kama vile Feisal na Mayele. Kwa upande wa Simba, pamoja na madhaifu mengine, kuna kaukweli kwenye kauli ya Kocha Pablo kuwa timu haifurukuti inapocheza mechi kubwa.

Yote kwa yote, mwaka huu zote haziko vizuri sana.
 
Kama ukawaida ni wenu tu msitujumuishe na maumivu yenu sema nyie ni wa kawaida,na tunajua ni wa kawaida tu
 
Hata wakiunganisha vikosi hawashindi kwa Azam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…